VANESSA AWANIA TUZO NYINGINE NCHINI CANADA


Tuzo za kimataifa kwa wasanii wa Tanzania zinazidi kuongezeka siku hadi siku. Vanessa Vee Money
anawania kipengele cha ‘Best International African Female Artist’ kwenye tuzo za African Entertainment Awards (AEA). Muimbaji huyo wa ‘No Body But Me’ ametoa taarifa hiyo kupitia akaunti yake ya Instagram.
“Namshukuru Mungu kwa nomination nyingine hii ya ‪#‎AEA‬ ya Canada. Ni Baraka kusema la ukweli Asanteni guys najua nguvu zenu pia zimechangia haya basi tupige kura. Link iko kwenye bio yangu Twitter @VanessaMdee ‪#‎AwardSeason‬”Tuzo hizo zitatolewa September 5, 2015 huko Mississauga, ambalo ni jiji la sita kwa ukubwa nchini Canada.

No comments:

Post a Comment