DR. SLAA AMEPEWA LIKIZO IKISHA ATAUNGANA  NA CHADEMA - MBOWE

Katika mkutano wa Baraza kuu la CHADEMA unaoendelea hivi sasa, Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman MBOWE amesema hakuna ugomvi na Dk. SLAA, amepewa likizo na ikiisha ataungana nao baadaye ili shughuli za Chama ziendelee.
Mbowe- Tumekubaliana Dr SLAA apumzike kwa muda na atakapokuwa tayari ataungana nasi mbele ya safari na nafasi yake ya ukatibu mkuu ndani ya chama iko pale pale
Mbowe- Chama hiki hatukiendeshi kwa siri, tunakiendesha kwa mikakati.
Mbowe- Tulilazimika kutumia kila mbinu halali ambayo inakiwezesha chama chetu kusaka matumaini na matarajio ya wananchi.
Mbowe- Tuliridhika
pasipo shaka kwamba ugeni wa Edward Lowassa katika chama chetu ni mpango wa Mungu.
Mbowe- Umoja wetu ndio ushindi, fursa iliyojitokeza ni nadra.
Mbowe- Mtikisiko huu umekuja kwa CCM kipindi ambacho Watanzania wanamatamanio ya mabadiliko
Mbowe- Hatuwezi kuwa chama cha kuendelea kuhubiri mabaya ya jana tukashindwa kuhubiri maendeleo ya kesho
Mbowe- Kipigo wanachopata CCM, hawajawahi kukipata tangu tuanze siasa za vyama vingi
Mbowe- Kila tunayeweza kumpokea kutoka vyama vilivyo nje ya UKAWA tutamchukua
Mbowe- Mungu ameamua kutumia chama chetu kujeruhi na kuangusha CCM.
Mbowe- CHADEMA ni chama cha siasa, ni chama makini, chama makinI ni chama cha watu, chama kisichokuwa makini ni chama cha viongozi.

No comments:

Post a Comment