Mlipuko wawaua watu 47 Nigeria

Jeshi nchini Nigeria linasema kuwa kumetokea mlipuko mkubwa katika soko moja kaskazini mashariki mwa jimbo la Borno ambapo watu 47 wamefariki huku wengine 55 wakijeruhiwa katika mji wa sabon gari.

Haijulikani iwapo mlipuko huo ulisababishwa na mlipuaji wa kujitolea muhanga ama kilipuzi kilichotegwa katika soko hilo.
Kundi la Boko Haram limekuwa likitekeleza mashambulio katika eneo lote la kaskazini mashariki mwa Nigeria.

No comments:

Post a Comment