Staa wa sinema za Kibongo, 
Elizabeth Michael ‘Lulu’  akiendelea ‘kujibebisha’ kwa staa wa Bongo 
Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
UCHOKOZI! Staa wa sinema za 
Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ anatengeneza kichwa cha habari kwa 
mara nyingine baada ya kudaiwa ‘kujibebisha’ kwa staa wa Bongo Fleva, 
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, kitendo kilichotafsiriwa kuwa ni 
kumchokonoa mwandani wa jamaa huyo, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’.
Tukio hilo lilijiri usiku mnene Jumapili
 iliyopita kwenye Ukumbi wa House Club uliopo Masaki, Dar ambapo 
kulikuwa na sherehe ya bethdei ya DJ wa Diamond, Rommy Jones.
Kwa mujibu wa shuhuda wetu aliyeweka 
kambi ukumbini humo, Lulu, bila kujali kwamba, Diamond alimwacha Zari 
nyumbani akimnyonyesha ‘baby girl’ wao, Latifah Nasibu a.k.a ‘Princess 
Tiffah’, alionekana akijiachia naye kimahaba huku akionesha ‘kummisi’ 
kinoma jamaa huyo.

Mastaa mbalimbali wakiwa katika sherehe hiyo.
ILIANZA HIVI
Lulu, alikuwa wa mwishomwisho kuingia 
ukumbini ambapo baada ya kuzunguka kusalimiana na mastaa wengine alitua 
kwenye sofa alilokuwa amekaa Diamond ambapo walianza kufanya yao bila 
kujali ëwavimba machoí waliokuwa wakiwakodolea.
Kwa kuwa Diamond alikuwa host 
(mwendeshaji) wa shughuli hiyo, Lulu alikuwa akimwaga mauno huku 
akimshangilia Diamond kufuatia muziki wake wa nguvu uliokuwa unarindima 
ukumbini humo.
Kutokana na hali hiyo, Lulu aliendelea 
kucheza zaidi kwa madai kwamba anaupenda mno muziki wa Diamond hasa 
ulipodondoshwa ule wa Mdogomdogo.

Diamond Platnumz akiwa na mpenzi wake Zari.
WAONESHANA MAHABA
Ilifika wakati Diamond alionekana 
akimpiga Lulu busu mdomoni huku watu wakishangilia ëoyoooí lakini wao 
hawakuwa wakijali chochote kwani waliendelea kufanya yao.
Kuna wakati walikuwa wakitaniana na 
kucheka huku wakigongesha glasi zao za mvinyo na kukumbushana mambo 
mbalimbali ya siku za nyuma.
Baadhi ya watu walisikika wakisema 
kwamba, Lulu anamchokonoa mama Tiffah ‘Zari’ kwani kwa usiku huo yeye 
alikuwa tu nyumbani akinyonyesha wakati baba mtoto wake akijiachia na 
kimwana huyo.
“Naona Lulu anatafuta matatizo kwa Zari 
kwani mahaba wanayooneshana hapa ukumbini siyo ya kawaida, yaani hawa 
mastaa wetu mbona majangaaa,” alisikika mmoja wa wahudhuriaji wa 
shughuli hiyo iliyokuwa ya kistaa kwani hakukuwa na ‘watoto wa mbwa’.
SHETTA AMWAGA FEDHA
Katika sherehe hiyo ilipambwa na mastaa 
kibao wa fani mbalimbali na mapedeshee wa mjini, walimmwagia Rommy mvua 
ya fedha huku mwanamuziki, Nurdin Bilal ‘Shetta’ akimzawadia fedha 
taslimu Sh. milioni moja ambapo shughuli iliendelea hadi majogoo.
Wakati hayo yakitendeka mmoja wa 
marafiki wa karibu wa Zari alimtumia ujumbe mfupi wa maneno (sms) 
kumfahamisha juu ya tukio hilo.
MASTAA KIBAO
Ukiacha Lulu na Shetta, baadhi ya mastaa
 wengine waliojiachia vya kutosha ni pamoja na Aunt Ezekiel na baba 
mtoto wake, Moses Iyobo, dada wa Diamond, Mwajuma Abdul ‘Queen Darleen’,
 Khaleed Mohamed ‘TID Mnyama’, Vanessa Mdee ‘Vee Money’ sambamba na Juma
 Musa ‘Jux’, Hamad Ally ‘Madee’, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ na wengine 
kibao.
LULU ANASEMAJE?
Akizungumzia hali hiyo, Lulu alisema 
kuwa ilikuwa ni pati na kupiga picha na Diamond haikuwa ishu kubwa kwani
 ni watu wengi waliopiga naye picha.
“Siamini wala sihisi kama Zari anaweza ‘kumaindi’ ishu kama hiyo. Kama akimaindi atakuwa na lake jambo,” alisema Lulu.
TUJIKUMBUSHE
Kabla ya tukio hilo, Lulu aliwahi 
kudaiwa kutoka na Diamond lakini alikanusha vikali ishu hiyo huku 
akionesha kuwa jamaa huyo hana ubavu wa kumsogelea wala kufaidi penzi 
lake.

No comments:
Post a Comment