Zitto kunguruma mkoani Dodoma leo

Kiongozi Mkuu wa chama cha ACT wazalendo Zitto Kabwe.
 Kiongozi Mkuu wa chama cha ACT wazalendo Zitto Kabwe, anatarajia kufanya ziara ya kukitambulisha chama hicho kwa
wananchi wa mkoani wa Dodoma leo. 
 
Katibu wa chama hicho mkoani hapa, Dennis Nyandwi, alisema jana kuwa ziara ya kiongozi huyo inalenga kukitambulisha chama hicho kwa wananchi wa mikoa 25 ya Tanzania, lakini katika awamu ya kwanza itakuwa na mikoa kumi.
 
“Katika mikoa kumi ya awamu ya kwanza na sisi Dodoma tupo hivyo tunajipanga katika kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa wakati wa ziara ya kiongozi wetu katika maeneo ya mkoa huu ambayo atafanikiwa kufika,” alisema Nyandwi.
 
Alifafanua kuwa viongozi wa ACT mkoa wa Dodoma watampokea kiongozi leo maeneo ya Gairo ambako nako atapita 
kuzungumza na wananchi.
 
Alisema baadaye leo Zitto ataelekea wilayani Bahi katika kijiji cha Chidilo ambako ataenda kufanya mkutano na kuzungumza na wanachi.
 
“Pia Zitto atatoa elimu ya uraia kwa wananchi wa kijiji hicho ili wajitokeze kwa wingi katika kujiandikisha kwenye Daftari la kudumu la wapigakura wakati ukifika,” alisema Nyandwi.
 
Baada ya kumaliza mkutano katika wilaya ya Bahi, atarudi mjini na kwenda katika kituo cha Radio ya Dodoma FM kuzunguza na wananchi na baadaye jioni  atakuwa na mkutano katika viwanja vya Mashujaa katika Manispa ya Dodoma.

No comments:

Post a Comment