Wajawazito waandamana.. mazishi ya pamoja waliofariki ajali ya basi.. na nyingine 7 kutoka MAGAZETINI leo APRIL 14

wats

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid.Zaidi ya akinamama wajawazito 70  katika kituo cha Afya cha Chikande, Manispaa ya Dodoma wameandamana hadi Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma kulalamikia  Rashid.Waziri wa Afya na
Malalamiko yao ni pamoja na kujifungulia njiani kutokana na kutembea umbali mrefu kwenda hospitali hiyo na baadhi yao kukataliwa kufunguliwa geti na walinzi wa hospitali wanapojisikia uchungu.
 
Martha Masine, alisema wameamua kuandamana ili kuwasilisha kilio chao kwa uongozi wa hospitali hiyo ili matatizo yao yatafutiwe ufumbuzi.
 
“Walinzi wa hospitali ya mkoa wamekuwa wakikataa kuwafungulia geti akina mama wanaofika hospitalini hapo usiku wakitokea Chikande na kusababisha baadhi ya wenzetu kujifungulia njiani na kuhatarisha maisha ya mama na mtoto anayezaliwa,” alisema Masine.
 
Alisema wamekuwa wakipata shida sana kufika hospitali hapo usiku, ingawa kituo hicho kipo nyuma ya hospitali.
 
“Tunaposhikwa na uchungu tunatembea  hata kama ni usiku ni hatari kutokana na njia kuwa ni vichochoro hadi kufika General (hospitali hiyo),” alisema.
 
Aidha, alisema wamekuwa wakisindikizana mmoja wao anaposhikwa na uchungu, lakini wanapofika hospitalini walinzi wanagoma kufungua mageti na kuwalazimu kurudi kituoni.
 
Alibainisha kwa nyakati mbili tofauti akiwa bado katika kituo hicho ameshuhudia akina mama wawili kujifungulia njiani kwa kutembea umbali mrefu kufuata huduma na mwingine kukataliwa na walinzi.
 
“Bado nipo katika kituo hiki nasubiria kujifungua, muda bado haujafika, lakini jamani sisi tunapata shida walinzi wa General wanapotukatalia kufungua mageti, huwa inatulazimu kuanza safari ya kurudi kituoni na kuna siku tukiwa njiani mwenzetu akajifungua tukamsaidia sisi tuliopo,” alisema Masine.
 
 Rose Atanas ambaye yupo katika kituo hicho akisubiria kujifungua, alisema changamoto nyingine ni kituo hicho kuzidiwa uwezo kutokana na kupokea akina mama wengi kutoka vijiji mbalimbali vya Mkoa wa Dodoma.
 
“Kituoni kuna kinamama wengi kuzidi uwezo wake, kituo kina vitanda 15 na hadi sasa kuna akinamama zaidi ya mia moja hali inayotulazimu kulala wawili wawili au watatu na wengine kulala chini na pia kuna wadudu watambaao kama vile kunguni na papasi,” alisema Atanas.
 
Alisema mbali na mrundikano huo pia unahatarisha afya zao na unatishia kuambulizwa na magonjwa ya kuambukiza.
 
“Pia tuna vyakula vyetu na kujipikia wenyewe kutokana na chakula tulichokuwa tukikipata kutoka hospitali ya mkoa kusitishwa bila ya kuambiwa sababu ya kufanya hivyo.
 
“Hapa tupo zaidi ya 100 kutoka wilaya mbalimbali za Mkoa wa Dodoma wengine tunalazimika kulala chini vitanda havitoshi, vyoo vyevyewe matundu yapo mawili na mabafu mawili yaani tukianza kuoga ni foleni na kwenda msalani ni foleni,” alisema Rose.
 
Akijibu malalamiko hayo, Muuguzi wa zamu katika hospitali hiyo, Sista Cesilia Sanya, aliwaahidi akinamama hao kuwa suala la walinzi kutofungua geti halitajirudia.
 
Hata hivyo, alisema hospitali imepokea malalamiko ya akina mama hao na walinzi waliobainika kufanya vitendo hivyo watachukuliwa hatua.
 
“Naomba niwahakikishie kwamba walinzi waliohusika kuwazuia watachukuliwa hatua kwa kuhatarisha maisha ya akinamama na watoto kwa kujifungulia njiani na hayo mengine nitayafikisha  sehemu husika,” alisema Sanya Kituo cha Chikande kilitengwa kwa ajili ya kuwalaza akinamama wajawazito wanaosubiri kujifungua  katika hospitali hiyo.

No comments:

Post a Comment