Ebola:Shule zafunguliwa Sierra Leone

Shule ambazo zimekuwa zimefungwa nchini Sierra Leone tangu mwezi Julai mwaka uliopita kutokana na mlipuko wa ugonjwa hatari wa Ebola zitafungwa hii leo jumanne.
Mataifa mengine yalioathirika na mlipuko huo wa Ebola Magharibi mwa Afrika Guniea na Liberia yaliruhusu kufunguliwa kwa shule zao mwanzoni mwa mwaka huu.
Shirika la afya duniani WHO limesema kuwa Ebola bado imebaki kuwa janga la kimataifa.

WHO inasema kuwa ugonjwa wa Ebola uliwaua karibu watu 10,600
Takwimu za hivi majuzi zinaonyesha kuwa kuwa ni visa vipya 30 vya ugonjwa wa Ebola vilivyothibitishwa nchini Guinea na Sierra Leone ikilinganishwa na mamia ya visa hivyo siku za nyuma.
WHO inasema kuwa ugonjwa wa Ebola uliwaua karibu watu 10,600 katika mataifa hayo ya Magharibi mwa Afrika.
Aidha WHO inasema kuwa jamii ya kimataifa inapaswa kuweka tahadhari kuu dhidi ya mlipuko huu ama mwengine wa Ebola.

No comments:

Post a Comment