TIGO YAZIDI KUWAWEZESHA WATEJA WAKE KUMILIKI BIASHARA ZAO WENYEWE KUPITIA PROMO YA BAJAJI‏


Mshindi wa droo ya 7 ya promosheni ya Tigo ‘Miliki Biashara Yako’ Bi. Linda Ndalu (28) akifurahia Bajaji yake mpya yenye thamani ya Tsh 6,700,000 mara baada ya kukabidhiwa katika hafla fupi iliyofanyika  Buguruni chama leo jijini Dar es Salaam.
Mtaalam wa masoko na biashara kutoka Tigo Bw. Gaudens Mushi (kushoto) akimpongeza Bi. Linda Ndalu (28) mjasiriamali, mkazi wa Sinza kwa kujishinda Bajaji katika promosheni ya ‘Miliki Biashara Yako’.

Mshindi wa droo ya 7 ya promosheni ya Tigo ‘Miliki Biashara Yako’ Bi. Rose Lukindo (45) ambaye ni mfanyakazi wa Manispaa wa Ilala akipokea darasa la jinsi ya kutumia Bajaji aliyoshinda kutoka kwa Mtaalam wa Masoko na Biashara Tigo Bw. Gaudens Mushi.
Mfanyakazi wa Manispaa ya Ilala Bi. Rose Lukindo (45) akionyesha ufunguo wa Bajaji mpya alioshinda katika promosheni ya Tigo ‘Miliki Biashara Yako’ mara baada ya kukabidhiwa zawadi hiyo mapema leo Buguruni Chama, jijini Dar es Salaam.
Mtaalam wa masoko na biashara kutoka Tigo Bw. Gaudens Mushi akimwelekeza mshindi wa promosheni ya ‘Miliki Biashara Yako’ Bw. Dotto Omari (33) kitufe cha kuwashia Bajaji mara baada ya kumkabidhi zawadi hiyo katika hafla iliyofanyika leo Buguruni chama, jijini Dar es Salaam.
Mtalaam wa Masoko na Biashara kutoka Tigo Bw,. Gaudens Mushi (kushoto) akimpongeza mshindi wa droo ya 7 katika promosheni ya ‘Miliki Biashara Yako’ Bw. Abdallah Abdallah (36) mkazi wa Mbezi anayefanya kazi za ufundi wa magari  mara baada ya kumkabidhi Bajaji yake katika hafla iliyofanyika leo Buguruni chama, jijini Dar es Salaam.
Mshindi wa droo ya 7 katika promosheni ya ‘Miliki Biashara Yako’ Bw. Abdallah Abdallah (36) mkazi wa Mbezi anayefanya kazi za ufundi wa magari akionyeshea ufunguo wa Bajaji aliyoshinda mara baada ya kukabidhiwa na Mtalaam wa Masoko na Biashara
Mtaalam wa masoko na biashara kutoka Tigo Bw. Gaudens Mushi (watatu kutoka kulia) akifurahi kwa pamoja na washindi wa promosheni ya Tigo ‘Miliki Biashara Yako’ waliokabidhiwa Bajaji zao leo Buguruni chama, jijini Dar es Salaam.
Wadau wa Tigo waliojikusanya maeneo ya Buguruni chama kwa ajili ya kushuhudia makabidhiano hayo ya Bajaji mapema leo.

No comments:

Post a Comment