
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry alisema kuwa Marekani ilitumia kemikali aina ya Sarin kushambulia wananchi
Hatua yoyote ya kijeshi 
itakayochukuliwa na Marekani dhidi ya Syria, huenda ikachochea usaidizi 
kwa wapiganaji waal-Qaeda na washirika wake kwa mujibu wa taarifa kutoka
 Damascus.
Naibu waziri wa mambo ya nje wa Syria, Faisal 
Mekdad pia aliambia BBC kuwa makundi ya wapiganaji waliojihami, 
yalitumia silaha za kemikali wala sio wanajeshi wa Syria.
Marekani awali ilisema kuwa ilikuwa 
na ushahidi wa kutosha kuonyesha kuwa serikali ya Assad ilitumia 
kemikali aina ya Sarin katika shambulizi baya sana wiki jana .
Rais Barack Obama ameahidi kuchukua hatua kali 
dhidi ya Syria lakini mwanzo anataka baraza la Senate kupigia kura hoja 
hiyo kabla ya kuchukua hatua zozote dhidi ya Syria.
Wabunge wa Marekani wanatarajiwa kukutana na 
maafisa wa ikulu ya White House huku maafisa hao wakiwa na imani kuwa 
wataunga mkono hoja ya Obama.
Hata hivyo hatua ya Obama mwanzo kutaka baraza 
la Senate kuunga mkono hatua ya serikali kutaka kushambulia Syria 
imewashangaza wengi hasa washauri wake wa karibu.
Sio wazi kuwa Obama ataungwa mkono hasa na wabunge wa bunge la waakilishi ambao wengi ni wa chama cha Republican.
Labda Pia kwenye Senate huenda asipate kuungwa mkono. Bila shaka hii itakuwa kura yenye wasiwasi kwa Obama.
Ikiwa Congress haitaunga mkono hoja ya Obama basi huenda, likawa jambo baya sana kwa utawala wake.
Tayari kamapeini imeanzishwa ya kuwashawishi 
watu nchini Marekani kuwa ni jambo jema kwa serikali ya Obama kuchukua 
hatua za kijeshi dhidi ya Syria.
Lakini kwa kukosa kuchukua hatua za mashambulizi
 na badala yake kuomba idhini ya baraza la Senate itakuwa mchezo wa pata
 potea kwa Obama.
No comments:
Post a Comment