Msanii
wa muziki wa Genge nchini Kenya,Paulo Julius Nunda a.k.a Jua Cali wiki
ijayo anatarajia kuachia ngoma yake iitwayo Kuna Sheng ambayo ameifanyia
remix ambayo hadi sasa mashabiki wa nchi hiyo wameipokea vizuri.
Ngoma
hiyo ataiachia baada ya kukaa kimya kirefu katika game hiyo na kwamba
maana ya jina la ngoma hiyo ni lugha ya mtaani,ikiwa na maana kuwa watu
kutoka mitaa mbalimbali kuwasiliana bila kujali tofauti zao ambapo ngoma
hiyo imetengenezwa na producer aitwaye Kanyeria.
Katika
Ngoma hiyo Jua Cali amewashirikisha wasanii mbalimbali kutoka katika mitaa ya Jiji la Nairobi kama Ummo, Kibera na Yeriko na wasanii hao ni Mkuu, Manchu, Virus, Vioxxi na Konkodi.
No comments:
Post a Comment