Keyboard hii inaweza kutumika katika tablets na smartphones.
-Ina upana wa nusu milimita kama karatasi-Ina uwezo wa kutumika katika tablets na smartphones kama 'touch screen'
-Ni wireless na inatumia umeme mdogo
Wanasayansi katika kampuni ya Cambridge 
Silicon Radio (CSR) wamevumbua keyboard nyembamba kuliko zote yenye 
upana wa nusu milimita sawa na karatasi. Keyboard hiyo ina uwezo wa 
kutumika hata katika tablets na smartphones kwa kuandika chochote, hivyo
 mtumiaji anaweza kuitumia kuandikia mesegi kwenye simu yake kama ilivyo
 kwenye 'touch screens'. Pia inaweza kutumika na karamu maalum kwa ajili
 ya kuandikia au kuchora michoro mbalimbali.
 
 


No comments:
Post a Comment