Home » Michezo » Unataka kufahamu gharama ya viwalo vya wachezaji ghali kuliko wote duniani?

Unataka kufahamu gharama ya viwalo vya wachezaji ghali kuliko wote duniani?

how does it cost
Wachezaji wakubwa duniani hulipwa fedha nyingi sana ambazo wakati mwingine hukufanya mtu wa kawaida kujiuliza jinsi ambavyo watu hawa hufanya matumizi ambayo yataendana na kipato wanachopata.

Wakati nyota wawili walioweka historia ya kuwa wachezaji ghali kuliko wote duniani walipokutana ndani ya uwanja wa mazoezi wa Real Madrid watu walijaribu kufananisha na kutoutisha baadhi ya vitu .
Ronaldo kama kawaida yake alikuwa ‘ametupia’ viwalo vya hatari akionekana nadhifu nah ii ni kawaida yake kwani Ronaldo kuna wakati huingia kwenye chumba cha kubadilishia nguo na mtaalamu wake wa nywele ili kumtengeneza nywele zake wakati wa Half Time.
Kwa upande mwingine Gareth Bale alionekana yuko kawaida kidogo tofauti na Ronaldo na ukawaida wake uliwafanya watu kudhani kuwa bado anahitaji kujifunza baadhi ya vitu toka kwa Ronaldo ili aweze kwenda sawa na nyota huyo hasa kwenye masuala ya mavazi .
Ronaldo alikuwa amevalia Jeans aina ya D Squared ambayo gharama yake ni paundi 325 , Begi la mkononi aina ya Gucci ambalo linauzwa paundi 265 ,miwani maalum ya jua ambayo thamani yake ni paundi 552 ,mkanda wa Dolce & Gabbana wenyewe unauzwa  paundi 450 na saa ya mkononi aina ya Jacob ambayo ni paundi 10,600. Jumla ya viwalo alivyotupia Cristiano kwa siku hiyo ni Paundi 12,192.
Ronaldo .
Begi la Gucci-265
Saa ya Jacob’s -10,600.
Belt ya Dolce &Gabanna -450.
Jeans ya D Squared-325.
Miwani ya macho-552.
Jumla-paundi 12,192/=
Saa aina ya Jacobs bei yake unaweza kununua gari aina ya Altezza au Mark II Grande GX 110 hapa Tanzania .
Saa aina ya Jacobs bei yake unaweza kununua gari aina ya Altezza au Mark II Grande GX 110 hapa Tanzania .

shades of grey
bag

Jeans aliyovaa Gareth Bale aina ya Dolce& Gabana.
Jeans aliyovaa Gareth Bale aina ya Dolce& Gabana.
Gareth Bale alikuwa ametupia vitu ambavyo thamani yake si kubwa sana , alikuwa amevaa Jeans ya Dolce & Gabana ya paundi 355 , Begi la mkononi la Louis Vuitton la paundi 420 , Tshirt ya Dolce & Gabana ya paundi 122 na kimfuko cha Nylon ambacho kinauzwa paundi 5 , kwa jumla Bale alikuwa ametupia pamba za paundi 902 .
Bale.
Jeans ya Dolce & Gabanna-355.
Begi Louis Vuitton-420.
Tshirt Dolce&Gabana-122
Mfuko wa Nylon-5
Jumla –Paundi 902/=
Story Za Michezo Kwa Hisani Ya Benki Ya NMB.

No comments:

Post a Comment