BINTI KIDATO CHA NNE: NIMEZAA NA DIAMOND


MREMBO aliyetimuliwa shule akiwa kidato cha nne baada ya kutundikwa mimba, Sasha Juma ameibuka na madai kuwa amezaa na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
MCHEZO MZIMA

Habari kutoka kwa chanzo chetu cha kuaminika zilidai kuwa Sasha na Diamond walikutana katika mgahawa mmoja uliopo kwenye maduka ya Mlimani City, Dar na ndipo walipoanzisha uhusiano.
Ilidaiwa kuwa Sasha akiwa na marafiki zake alitoka kwenye moja ya maduka hayo ambapo alimkuta Diamond na binamu yake, Romy Jones wakiwa wamekaa nje ya mgahawa huo.
Ilidaiwa kwamba kwa kuwa Sasha anajuana na Romy muda mrefu, aliwafuata kisha akawasalimia ndipo Diamond akaonekana kuvutiwa na mrembo huyo na kumwambia kuwa atachukua namba yake ya simu ya kutoka kwa Romy kwa vile alikuwa nayo.
Chanzo chetu hicho kilizidi kutiririka kuwa baada ya hapo Sasha aliondoka na marafiki zake, kipindi hicho akiwa anasoma kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Dar es Salaam International iliyopo Sinza-Kumekucha, Dar.
WAKUTANA
Ilidaiwa kuwa Diamond alianza kuchati na Sasha kabla ya kukutana na ‘kufanya yao’.
Shushushu huyo alitonya kuwa Sasha na Diamond walikutana Sinza-Palestina, Dar wakati huo mwanamuziki huyo alikuwa akimiliki gari aina ya Toyota Opa.
WEMA ATAJWA
Ilidaiwa kuwa Sasha alipotimba eneo la tukio aliingia ndani ya gari la Diamond na kuongea naye kuhusu mapenzi ambapo msanii huyo alimwambia kitu ambacho alichovutiwa kwake ni jinsi mrembo huo alivyofanana na Wema Isaac Sepetu ambaye aliwahi kuwa mwandani wa jamaa huyo.
Madai yalizidi kushushwa kuwa baada ya mwanamuziki huyo na Sasha kukubaliana walipanga kuonana kesho yake katika hoteli moja maarufu iliyopo Sinza-Madukani, Dar ambapo msanii huyo alimwambia mrembo huyo atangulie atapewa ufunguo na kuoneshwa chumba na wahudumu.
Ikasemekana kwamba baadaye Diamond alifika na kuungana na wenzake chumbani.
Ilidaiwa kuwa jamaa alipotimba chumbani alimbebea ‘mtoto’ kinywaji laini aina ya Saint Anna.
‘Niuzi’ za chumbani zilidadavuliwa kuwa wakati wakiendelea kupiga kinywaji mdogomdogo ndipo staa huyo akaomba ‘mchezo’.
Ilisemekana kuwa Sasha alileta zile za ‘nataka sitaki’ lakini baadaye alimsihi kwa nguvu zote watumie kinga ambapo mwanamuziki huyo alimwambia asijali hawezi kumpa mimba kuna mbinu ataitumia.
Chanzo hicho kiliendelea kushusha madai kuwa baada ya kumaliza mambo yao, Diamond alimchukulia Sasha usafiri wa Bajaj na kumpa shilingi elfu 80 na kumwambia kuwa wataendelea kuwasiliana.
Ilidaiwa kuwa mawasiliano yaliendelea ambapo mwezi mmoja na nusu baadaye, Sasha alianza kujisikia vibaya  na walipopanga kukutana mara ya pili, mrembo huyo alimweleza jinsi anavyojisikia ambapo Diamond alinunua kipimo cha kupimia mimba na kukuta tayari Sasha alishanasa.
Ilielezwa kuwa baada ya kuona hivyo Diamond alimsihi Sasha asitoe ujauzito huo na kumwambia kuwa akifanya hivyo anaweza kufa na kama atajifungua yeye (Diamond) atamsomesha mrembo huyo na kumlea mtoto wao.
Mpashaji wetu aliendelea kusema kuwa baada ya kuachana hapo, waliendelea kuwasiliana japo siyo kama mwanzo na baadaye mawasiliano yalikatika kabisa huku Sasha akiwa tayari amefukuzwa shule. Mama yake Sasha alijaribu kumpigia simu Diamond lakini msanii huyo akawa anajibu kuwa atawasiliana naye baadaye, jambo ambalo hakuwa akilitimiza hadi alipojifungua mtoto wa kike katika Hospitali ya Mwananyamala, Dar na kumpa jina la Rujeina.
SASHA AKIRI
Baada ya kupata madai hayo, gazeti hili lilimsaka Sasha ili kuthibitisha ambapo mwanzo alisita kuzungumza lakini baadaye akakiri kuzalishwa na mwanamuziki huyo na kudai kuwa kwa kuwa hamjali tena,  naye aliacha kumfuatilia.
“Ni kweli nimezaa na Diamond. Mtoto ana miezi mitatu sasa. Unajua yeye ndiye alinikatisha masomo na kusema kuwa ataniendeleza na atamlea mtoto hivyo alivyokaa kimya sikuona tena sababu ya kumfuatilia kwa vile kwetu napata kila kitu,” alisema Sasha.
Alipotafutwa Diamond kupitia simu ya kiganjani akiwa Nairobi, Kenya na kupewa nafasi ya kusema ukweli juu ya ishu hiyo, alieleza:
“Hahahaaa…mbona hiyo ishu ni kubwa sana kwangu! Ukweli huyo mwanamke simjui kabisa. Lete stori nyingine achana na hiyo.”
Katika kuonesha ‘usiriazi’, gazeti hili liliendelea kumbana Diamond lakini bado alizidi kumkana Sasha.

No comments:

Post a Comment