
MASKINI Daz Baba! Ndivyo unavyoweza kusema kufuatia habari ya kusikitisha ya msanii huyo ambaye jina lake kamili ni David Jacob kunaswa akiwa amezima mjini hapa huku ulevi wa kupindukia ukidaiwa kuwa chanzo.
Daz Baba au Daz Mwalimu asubuhi ya Agosti 5, mwaka huu alinaswa na kamera za gazeti hili akiwa hajitambui kwenye eneo maarufu kwa jina la Itigi lililopo nje ya Stendi ya Mabasi ya Msamvu ikidaiwa kuwa alifika mitaa hiyo tangu usiku wa jana yake.
“Huyu atakuwa amelewa sana na inawezekana katumia madawa ya kulevya au kawekewa madawa kwenye bia. Dah! Inasikitisha sana kwa msanii kama huyu ambaye huko nyuma alikuwa aking’ara kwenye anga la muziki,” alisikika akisema kijana mmoja aliyekuwa eneo hilo.
Hata hivyo, jitihada za kumuamsha ziligonga ukuta na mpaka paparazi wetu anaondoka eneo la tukio bado msanii huyo alikuwa hajitambui na mfukoni hakuwa na kitu, ikiashiria kuwa wahuni walimkomba kila kitu.
No comments:
Post a Comment