Moyes aanza kazi kwa ushindi.

CS3


Kocha wa Manchester United David Moyes hii leo ameanza rasmi kibarua chake kama kocha wa timu hiyo kwenye mechi ya ushindani baada ya kuiongoza timu hiyo kupata ushindi wa wa mabao mawili kwa bila katika mchezo wa kuwania ngao ya jamii dhidi ya Wigan Athletic .
United ilifunga mabao yake kupitia kwa mfungaji bora wa ligi kuu ya England kwa msimu uliopita Robon Van Persie ambaye alifunga mabao yote mawili .
United iliingia kwenye mchezo huo bila mshambuliaji wake Wayne Rooney ambaye hakuchaguliwa kwa kuwa ni majeruhi huku mustakabali wake ndani ya klabu hiyo ukibakia kuwa kitendawili .
CS 1

Beki wa Manchester United ambaye pia ni nahodha msaidizi wa timu hiyo Mfaransa Patrice Evra alikuwa mchezaji bora wa mchezo huo baada ya kucheza kwa kiwango cha juu ambapo alichangia kwenye ufungaji wa mabao yote mawili.
Taji la Ngao ya Jamii linakuwa taji la kwanza kwa kocha mpya David Moyes tangu alipoteuliwa kurithi nafasi ya kocha wa zamani Sir Alex Ferguson mwishoni mwa msimu wa ligi ulioisha .
David Moyes ataanza rasmi kampeni ya utetezi wa ubingwa wa ligi kuu ya England kwa klabu yake wiki ijayo wakati Manchester United watakapovaana na Swansea City kwenye mhezo wao wa kwanza wa ligi .
Story Za Michezo Kwa Hisani Ya Benki Ya NMB.

No comments:

Post a Comment