DRC yailemea Cameroon katika mechi ya CHAN

Timu ya taifa ya Cameroon
Matumaini ya Cameroon ya kufuzu kwa fainali ya kombe la mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaoshiriki ligi ya nyumbani CHAN, itakayoandaliwa nchini Afrika Kusini, imedidimia baada ya kulazwa bao moja kwa bila na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Bao hilo la pekee la na ushindi lilitiwa kimyani kunako dakika ya sabini na Mubele Ndombe ambaye anaichezea klabu ya Vitalo.
Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambayo ilishinda kombe hilo kwa mara ya kwanza mwaka wa 2009, ilitawala mechi hiyo na kwa sasa wanapigiwa upato kufuzu kwa fainali hiyo.
Cameroon na DRC zilishindwa katika mechi zao za kufuzu za mashindano yaliyopita katika kanda ya kati, huku Cameroon ikishindwa na Gabon nayo Congo ililemewa na majirani wao Congo-Brazzaville.
Mechi hiyo ilihairishwa kutoka siku ya Jumapili na kucheza Jumatatu usiku baada ya refa wa mechi hiyo, raia wa Sudan kukosa kufika kwa wakati.
Mechi ya raundi ya pili itachezwa mjini Lubumbashi mwishoni mwa juma hili ili kumua timu itakayofuzu kwa hatua ijayo ya fainali hizo za CHAN.

No comments:

Post a Comment