CLOUDS MEDIA GROUP YAANDAA SEMINA YA FURSA MKOANI TABORA LEO

Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya, Diamond, akiwaimbisha washiriki wa semina ya Fursa waliojitokeza kwa wingi mapema leo kwenye ukumbi wa Student's Center uliopo katikati ya mji wa mkoa wa Tabora, kushoto kwake ni Bwa. Marco Vingila kutoka shirika la TPSF.

Baadhi ya Wasanii wa muziki wa kizazi kipya wakishiriki semina ya Fursa kwa vijana ililiyofanyika leo kwenye ukumbi wa Student's Center katikati ya mji wa mkoa wa Tabora mapema leo, kutoka kulia ni Msanii Godzilla, Baba Levo, Amin, Stamina na wengineo.
Mkuu wa Masoko na Mauzo wa kampuni ya mafuta-Lake Oil, Bw Ben Temu akizungumza kwenye semina ya Fursa, ambapo yeye alielezea mambo mbalimbali ikiwemo suala la vijana kuwa wenye moyo wa kujituma na kutokata tamaa, alieleza kwa kuwataka vijana wawe wavumilivu na kutoka tamaa kwa kila fursa wanayokumbana nayo,badala yake waitumie vizuri katika suala zima la kujikwamua na kujiendeleza kimaisha. Semina hiyo iliyoandaliwa na Clouds Media Group, imefadhiriwa na shirika la NSSF; Zantel, MaxMalipo, Lake Oil.
Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji kutoka Clozds Media Group,Ruge Mutahaba,akizungumza mbele ya washriki wa Semina ya Fursa ndani ya ukumbi kwenye ukumbi Student's Center uliopo katikati ya mji wa mkoa wa Tabora.
Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya, Mwasiti Almas akizungumzia baadhi ya fursa alizozipata mara baada ya kujiunga na shirika la NSSF, mbele ya Washiriki wa Semina ya Fursa (hawapo pichani), kulia kwake ni Mwakilishi wa NSSF-Makao Makuu Bw. Salim Khalfan akimsikiliza kwa makini. Semina hiyo iliyoandaliwa na Clouds Media Group, imefadhiriwa na shirika la NSSF; Zantel, MaxMalipo, Lake Oil.


No comments:

Post a Comment