DIAMOND, MKENYA... PENZI UPYAA

Na Musa Mateja
MWANAMUZIKI Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amegeuka gumzo nchini Kenya baada ya mrembo mmoja aliyejipatia jina kupitia Runinga ya KTN, Angel Maggy kutangaza penzi lao upya kwa mara nyingine.

Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akipozi na Angel Maggy.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari za burudani vya Kenya, mara baada ya Diamond kufanya shoo mbili katika Miji ya Nairobi na Mombasa nchini humo, alipogeuza kisogo kurejea Bongo ndipo ukaibuka mlipuko wa habari zilizomhusu na mrembo huyo.
Ukiachilia mbali gumzo la vurugu zilizotokea baada ya Diamond kucheleweshwa kupanda stejini na kusababisha watu kupigwa chupa huko Mombasa, kilichofuata ni skendo ya mapenzi na mrembo aliyepata jina kupitia kipindi cha Tujuane cha KTN.

APOKELEWA KWA BASHASHA
Habari hizo zilieleza kuwa mara tu baada ya kutua nchini humo, Diamond alipokelewa kwa bashasha na mrembo huyo akiwa na wenzake wanne.
Ilielezwa kuwa tofauti na warembo wengine, Angel alimganda Diamond kila kona kuanzia akiwa jijini Nairobi katika shoo yake ya kwanza na siku ya pili aliambatana naye hadi Mombasa kwenye shoo ya pili.

Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz' akijiachia na warembo akiwemo Angel  wa pili kulia.
DEDICATION
Ilisemekana kuwa alipokuwa akifanya shoo kwenye Ukumbi wa KICC, Nairobi siku ya kwanza, Diamond aliimba wimbo wake wa Ukimuona maalum (dedication) kwa ajili ya Angel, jambo lililomfanya mrembo huyo kuonekana ‘spesho’ miongoni mwa maelfu waliohudhuria onesho hilo.
Imeripotiwa kuwa baada ya shoo hiyo kumalizika ‘naiti’ kali, Angel alionekana ‘beneti’ na Diamond wakielekea katika hoteli aliyofikia staa huyo Nairobi.
Hata hivyo, hakuna mahali palipoelezwa kama walilala wote usiku huo.
Habari zilizidi kutonya kuwa kesho yake mrembo huyo alionekana kila kona aliyokatiza Diamond mjini na baadaye kwenye shoo ya Mombasa ambako huko ndiko kulipotawaliwa na vituko vya kufa mtu.
Diamond.
MAHABA KULIKO WEMA!
Ilidaiwa kuwa kwenye shoo hiyo ndiko Angel alipokuwa akiahidi kumpa Diamond mahaba mazito kupitiliza yale aliyokuwa akipewa na zilipendwa wake, Wema Isaac Sepetu kwa kuwa wanamjua.

AJIPACHIKA DEMU WA DIAMOND
Ikasemekana kuwa wakati Mkenya huyo akitamba kwa mara nyingine kuwa ndiye demu wa Diamond na kupewa jina hilo (Demu wa Diamond), warembo wenzake walikuwa wakimuonea wivu kwa kuwa mwanamuziki huyo ni gumzo kwa wanawake nchini humo.
Diamond akiwa na Penny.
MASHEMEJI WAMKUBALI
Ilidaiwa kuwa wakati Angel akijitapa kuwa ndiye malkia mbele ya mfalme Diamond, mashosti zake waliojiita mashemeji, nao walikiri kumkubali mwanamuziki huyo.
Ilisemekana kuwa Angel na wenzake walimbatiza Diamond jina la Mfalme wa Afrika Mashariki hasa alipofanya shoo iliyowaacha watu hoi kwa namna alivyokonga nyoyo zao.

WALILALA WOTE?
Baada ya shoo kuliibuka madai mazito kuwa Angel alipata nafasi adimu ya kwenda kulala na Diamond katika hoteli aliyofikia huko Mombasa Beach.

WANAKUMBUSHIA?
Iliendelea kufahamika kuwa wawili hao hawakuonesha ugeni wa kuonana kwani walionekana ni watu waliozoeana kwani mara kadhaa Angel wa Diamond alinukuliwa akisema yeye ndiye malkia wa staa huyo wa Wimbo wa Kesho.
“Wanaonekana kuzoeana kwa sababu mwaka jana walikutana Mombasa ‘so’ siyo mara yao ya kwanza, wanakumbushia, sema tu safari hii imekuwa ‘too much’,” ilisomeka sehemu ya habari hiyo.

AJICHORA ‘TATTOO’
Katika kuonesha kuwa kuna kitu kati ya wawili hao, Angel amejichora ‘tattoo’ ya jina la Diamond na alama za ‘malavu’ kwenye mkono wa kushoto huku rafiki zake wakidai kuwa ana nyingine ya mwanamuziki huyo aliyojichora sehemu nyeti.

BOFYA HAPA KUMSIKIA DIAMOND
Baada ya kuwepo kwa habari hizo ambazo hakuna mahali Diamond alipopewa nafasi ili kupata mzani wake, gazeti hili lilimtafuta Diamond na kumpa A-Z ambapo alikiri kumfahamu Angel na kufunguka anachokijua.
“Namjua (anatajiwa Angel), kila nikienda huko huwa anapenda kuwa na mimi. Nilipofika kule (Nairobi) niliandaliwa mamodo ambao nilikwenda nao Mombasa na huyo mrembo alikuwa mmoja wao.
“Alinionesha hata hiyo tattoo akaniambia ananipenda sana na ndiyo maana kajichora jina langu.

“Kweli kuna picha tulipiga, huwa huyo mrembo anajitangazia huko Kenya kuwa anatoka na mimi kimapenzi ila si kweli namjua tu kawaida,” alisema Diamond kwa makubaliano kuwa akimaliza shoo ya Fiesta leo mkoani Tabora atatafuta chansi kulizungumzia sula hilo kwa kina.

Penny.
PENNY HAJUI KITU
Gazeti hili halikuishia hapo kwani lilimsaka mchumba wa Diamond, Peniel Mungilwa ‘Penny’ ili kujua kama anajua chochote kuhusiana na ishu.
Hata hivyo, simu ya Penny haikupatikana hewani lakini kwa mujibu wa rafiki yake wa karibu, mrembo huyo hajui chochote kinachoendelea.

HUKO NYUMA
Septemba mwaka jana, gazeti tumbo moja na hili, Risasi Jumamosi liliripoti habari ya Angel kujitapa kulala na staa huyo alipokwenda nchini humo kwa ziara ya shoo ambapo Diamond alisikitishwa na kitendo hicho hivyo habari hii ni mwendelezo wa madai ya mrembo huyo kuwa penzi lao limeibuka upya.

No comments:

Post a Comment