Rais Barack Obama na waziri wake wa zamani wa mambo ya nje Hillary
Clinton wameunganisha nguvu katika kampeni wakati Clinton akitafuta
nafasi ya urais wa Marekani na rais huyo wa sasa akijaribu kumhakikishia
kwamba sera zake zinapita urais. Obama alitoa hotuba ya hisia akieleza
kwanini anaamini wamarekani wamchague Clinton kuwa rais wa 45 wa
Marekani.
“Nina shauku kubwa, Hillary amenipa shauku na niko tayari kufanya kazi!aliuambia umati wa watu waliokuwa umevutiwa mno huko Charlotte ,North Carolina Jumanne.
Obama alimwelezea waziri wake wa mambo ya nje wa zamani kuwa ni mtu mwenye uelewa mkubwa , mwenye uwezo mkubwa, anayefanya kazi kwa bidi, mwenye maamuzi magumu na kiongozi anayependa kazi yake ambaye atalinda taifa kusaidia familia zinazofanya kazi na kuinua thamani na matakwa ya Marekani.

No comments:
Post a Comment