Mfungwa wa zamani Guantanamo Bay akamatwa


Airat Vakhitov Mfungwa wa zamani katika jela ya Guantanamo Bay Cuba.
Airat Vakhitov Mfungwa wa zamani katika jela ya Guantanamo Bay Cuba.
Mfungwa wa zamani katika jela ya Guantanamo Bay Cuba ni kati ya watu 30 ambao maafisa wa Uturuki wanasema wamewakamata kwa kuhusiana na mashambulizi ya wiki iliyopita ya kigaidi katika uwanja wa ndege wa Ataturk Instanbul.
Chanzo cha habari ndani ya jumuiya ndogo ya waislam ya kaskazini mwa Uturuki aliiambia VOA kimeeleza kwamba Airat Vakhitov ambaye alikaa miaka miwili katika gereza la Guantanamo Bay baada ya kukamatwa na majeshi ya Marekani 2001 huko Afghanistan alikamatwa Jumanne.
TONYTZ.BLOG haina uthibitisho wa kukamatwa kwake kutoka kwa serikali ya Uturuki.
Jumanne vyombo vya habari vya magharibi vilikariri maafisa wa serikali ya Uturuki wakisema idara ya usalama ya nchi hiyo imekamatwa watu 30 waliohusika katika mashambulizi hayo ya kigaidi, ambayo Ankara wanaamini ilikuwa ni kazi ya kundi la Islamic State. Kwa mujibu wa vyanzo vya habari vya serikali ya Uturuki 11 kati ya waliokamatwa ni raia wa Russia.

No comments:

Post a Comment