MULTICHOICE YAJA NA DSTV BOMBA, DIAMOND ALA SHAVU

MULTICHOICE (1) 

 Meneja Mipango wa DStv, Baraka Shelukindo, akifafanua jinsi huduma ya Dstv Bomba inavyofanya kazi.

MULTICHOICE (4) 

 Balozi wa DStv Bomba, Diamond Platnumz akisistiza jambo wakati akiwataka wananchi kujanjaruka na kutumia huduma za DStv na kutozihofia kama zamani kwa kuhisi ni huduma za watu wa kipato cha juu.MULTICHOICE (2) 

Mapaparazi na wadau wengine wakisikiliza maelezo yaliyokuwa yakitolewa kuhusiana na huduma hiyo.
MULTICHOICE (3) 
 Mkutano ukiendelea.
KAMPUNI ya MultiChoice Tanzania leo imezindua king’amuzi kipya cha DStv Bomba ambapo mteja atapata chaneli 65 ikiwemo huduma ya vituo kadhaa vya televisheni za hapa nchini. Katika chaneli hizo kuna vipindi mbalimbali ikiwemo taarifa za habari, muziki na filamu za Kibongo, michezo, dini, vipindi vya watoto, wanawake, wanaume, mitindo n.k.
kizungumza kwenye uzinduzi huo, Meneja Masoko wa kampuni hiyo, Furaha Samaru, alimtaja msanii wa muziki wa Kibongo Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kuwa balozi wa king’amuzi hicho na kutaja gharama zake kuwa ni shilingi 23,500/= kwa mwezi na king’amuzi chenyewe kinapatikana kwa shilingi 79,000/= na kuwataka wananchi kuchangamkia huduma hiyo.
Samaru alisema king’amuzi hicho kimeshasambaa nchi mbalimbali barani Afrika hivyo wasanii wa filamu, muziki na wengineo ambao watang’aa kwenye vipindi hivyo watakuwa wakionekana pande mbalimbali barani Afrika na hivyo kuwapatia umaarufu na kuwaongezea soko la kazi zao.


 

No comments:

Post a Comment