SILI NZITO KUHUSU DK. SLAA KUMKATAA LOWASSA UKWELI NI HUU


Na waandishi Wetu
 

NIkweli, ukweli ni huu! Wakati maelfu ya watu nchini wakiamini kutoonekana hadharani kwa Katibu Mkuu
  http://globalpublishers.co.tz/wp-content/uploads/2015/07/slaa.jpg
wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibroad Slaa kunatokana na kuchukizwa na kitendo cha kukaribishwa kwa waziri mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa na kupewa fomu ya kuwania urais kupitia chama hicho, ukweli wa jambo hilo umeibuliwa, TONYTZ.BLOG inakupa zaidi.
 Edward Lowassa na alipochukua fomu ya kuwania urais kupitia Chadema.
Mjumbe mmoja wa Kamati Kuu (CC) ya chama hicho, aliyeomba hifadhi ya jina lake, ameliambia gazeti hili kuwa, madai yanayotolewa na watu mitaani na katika mitandao ya kijamii yakisema Dk. Slaa amekasirishwa na kitendo hicho ni ya uongo.
ALIANZA DK. SLAA, MBOWE MH!
Mjumbe huyo alisema kuwa, Dk. Slaa ndiye mtu wa kwanza ndani ya Chadema kutoa wazo na hatimaye kushiriki kikamilifu katika vikao vya kumwezesha Lowassa kujiunga na chama hicho.
“Kwa taarifa yako, Dk. Slaa ndiye aliyemtaka Lowassa ajiunge Chadema. Mbowe (Freeman, Mwenyekiti wa Taifa Chadema) hakumtaka kabisa huyu jamaa aje kwetu. Kwa sababu hakuona jinsi gani wangewaeleza wananchi juu yake, lakini mzee ndiye aliyeshawishi na vikao vya kumjadili vikaanza mfululizo. Ukiangalia picha za awali, Dk. Slaa yupo.”
MTOA HABARI ASHIRIKI VIKAO
“Mimi ninayekwambia ni Mjumbe wa Kamati Kuu, nimeshiriki zaidi ya vikao 14 vilivyokuwa vikimjadili Lowassa na vyote hivyo, Dk. Slaa alikuwepo. Huyu jamaa hajakaribishwa kwa utashi wa mtu mmoja kama mnavyosikia huko nje na wala mzee Mtei (Edwin, mwasisi wa chama hicho) hahusiki na chochote,” alisema mjumbe huyo.
WABUNGE WAKOROFI WALIAFIKI
Kwa mujibu wa mjumbe huyo, ili kuondoa dhana kuwa, Lowassa anapelekwa Chadema na uongozi, wabunge wote ‘wakorofi’ ndani ya chama hicho walikaribishwa kushiriki vikao 14 vya kumjadili ili pia wamuulize maswali na yapate majibu kitu ambacho kilifanyika kwa ufanisi wa hali ya juu.
Aliwataja baadhi ya wabunge hao ‘wakorofi’ na majimbo yao kwenye mabano kuwa ni pamoja na Godbless Lema (Arusha Mjini), John Mnyika (Ubungo), Tundu Lissu (Singida Mashariki), Joseph Mbilinyi (Mbeya Mjini), Halima Mdee (Kawe), Peter Msigwa (Iringa Mjini), Joshua Nassari (Arumeru), Ezekiel Wenje (Nyamagana),  David Silinde (Mbozi Magharibi) na Highness Kiwia (Ilemela).
“Unajua, kwa vyovyote vile, vikao kama vingefanywa na viongozi wa juu peke yao, hawa wabunge wakorofi wangesumbua sana, lakini wote walishiriki na hakuna ambacho hawakijui. Ndiyo maana wote wamekaa kimya kwa sababu taratibu zote zilifuatwa,” alisema mjumbe huyo.
UKWELI ULIVYO
“Hapa lazima nikueleze ukweli. Kinachotokea kwa Dk. Slaa ni shinikizo kutoka familia yake. Kuna watu walikuwa na matumaini makubwa ya kufaidika endapo yeye angegombea tena na kushinda urais mwaka huu, hivyo wameamua kununa kwa sababu kilichotokea hakina masilahi kwa familia.
YADAIWA DK. SLAA ALITAKIWA KUCHAGUA MOJA
Mjumbe huyo alikwenda mbali kwa kusema kuwa, wakati wa mchakato wa Dk. Slaa kutaka Lowassa aingie Chadema baada ya kukatwa jina na Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mjini Dodoma, hakuiambia familia yake mpaka dakika za mwisho, ikajulikana.
“Ndipo familia ikamweka chini na kumwambia achague moja. Aendelee na siasa za Chadema au aachane  na siasa hizo ili  aangalie familia yake kwani kitendo chake cha kuwa mstari wa mbele kumtaka Lowassa kiliashiria kuwa, yeye hatagombea tena urais hivyo kuua matumaini ya familia. Ndiyo maana yupo kimya na hafiki ofisini.”
CHADEMA YAPANGA SAFU YA KUMSHAWISHI
“Sasa dokta ni mtu mzima. Hawezi kuliamua hilo kirahisi kama unavyofikiria. Ni lazima aende nalo taratibu ili kuziridhisha pande zote mbili. Na kwa kutambua hilo, chama kimeunda jopo la watu, wakiwemo mapadri, mashehe na marafiki zake ili wamshawishi arejee Chadema lakini akiiweka familia yake katika kuridhia na kumwelewa,” alisema mjumbe huyo wa Kamati Kuu.
LOWASSA AANIKA UKWELI KUHUSU RICHMOND
Kuhusu madai ya muda mrefu ya chama hicho yanayomtaja Lowassa kuwa ni fisadi, mjumbe huyo alisema kiongozi huyo aliwaeleza kwa ufasaha kuhusu utajiri wake na wakaridhika. Kwa upande wa Richmond, aliwaeleza kuwa alishataka kuuvunja mkataba huo, lakini mamlaka ya juu ikamzuia.
TAASISI TOKA NJE YATUA NCHINI KUTAFITI
Juu ya nafasi yao kushinda urais wakiwa na Lowassa, mjumbe huyo alisema kabla ya kuafiki kumtangaza kugombea, kwa gharama za Chadema, walikodi taasisi ya utafiti kutoka nchini Ujerumani kuja Tanzania ili kufanya utafiti nchi nzima kama Lowassa anakubalika.
Alisema utafiti ulipokamilika, ikaonesha kuwa, kama uchaguzi mkuu ungefanyika Julai 2015, Lowassa alikuwa mbele ya wagombea wenzake kwa asilimia 65.
SLAA KIMYAAA!
Hadi gazeti hili linakwenda mtamboni, Dk. Slaa hajajitokeza kuelezea kilichosababisha ukimya wake huku akiwa hapokei simu ya Uwazi kitu kinachozidisha kwa kasi maneno mitandaoni juu ya hatima yake ndani ya chama hicho kikuu cha upinzani.
Alhamisi iliyopita gazeti dada na hili, Uwazi Mizengwe linalotoka kila Ijumaa, waandishi wake walishinda nyumbani kwa Dk. Slaa, Mbweni nje kidogo ya Jiji la Dar lakini walishindwa kuongea naye licha ya kumpelekea karatasi yenye ujumbe wa kumuomba kuzungumza naye, waliambulia kumuona kwa mbali akiwa ndani ya geti la nyumba yake.LOWASSA

No comments:

Post a Comment