Ronaldo Amzawadia Wakala Wake Zawadi Ya Kufuru

Ronaldo Amzawadia Wakala Wake Zawadi Ya KufuruBilionea wa kilabu ya Real Madrid nyota Cristiano Ronaldo amempa wakala wake Jorge Mendes kisiwa kimoja cha Ugiriki kama zawadi yake ya harusi kulingana na vyombo vya habari.

Kisiwa hicho hakijatajwa lakini thamani yake huenda ikawa ya mamilioni kulingana na ripoti hizo.
Kulingana na mtandao wa michezo wa Uhispania Mundo Deportivo,Ronaldo anakijua kisiwa hicho kutokana na ziara zake wakati wa likizo.
Bwana Mendes alimuoa mshirika wake Sandra nchini Ureno siku ya jumapili.

Alex Furguson ni miongoni mwa wageni waliohudhuria harusi hiyo.
Furguson ambaye alikua meneja wa  klabu ya Manchester United alimsajili Ronaldo mwaka 2003 na mshambuliaji huyo wa Ureno ni mmoja ya wachezaji bora duniani alihudumu katika kilabu hiyo ya Old Trafford hadi mwaka 2009.
Ronaldo ameshinda taji la Ballon d’Or kama mchezaji bora wa mwaka mara tatu.

No comments:

Post a Comment