Nay Wa Mitego afunguka uhusiano wake na Shamsa Ford
    
        
                    
                 
Staa wa Bongo Fleva,Elibarik Emmanuel ‘Nay Wa Mitego’amefunguka 
uhusiano wake na mwigizaji wa filamu za Kibongo,Shamsa Ford baada ya 
picha kadhaa kuzagaa mtandaoni wakiwa kimahaba wakipigana mabusu.Akipiga 
 Stori na TONYTZ.BLOG alisema kuwa hana uhusiano wa kimapenzi na mwanamke 
yoyote kwa sasa siyo tu Shamsa Ford, na nafasi ipo kwa yoyote 
anatakayekubali kuwa mpenzi wake. ‘’Jamani nipo singo kwa sasa sina uhusino na mwanamke yoyote na Shamsa 
siyo mpenzi wangu,’’alisema Nay. Akizungumzia picha zilizozagaa 
mtandaoni akipigana mabusu na mwigizaji huyo alisema kuwa hiyo ni filamu
 yao mpya ya kimapenzi ambayo itatoka muda si mrefu kuanzia sasa.
‘’Jamani nipo singo kwa sasa sina uhusino na mwanamke yoyote na Shamsa 
siyo mpenzi wangu,’’alisema Nay. Akizungumzia picha zilizozagaa 
mtandaoni akipigana mabusu na mwigizaji huyo alisema kuwa hiyo ni filamu
 yao mpya ya kimapenzi ambayo itatoka muda si mrefu kuanzia sasa.
 
‘’Ile picha ni vipande vya movie yetu ya kimapenzi mimi na Shamsa bado 
hatujaipatia jina kwa sasa mashabiki wasubiri tu wataiona halafu Shamsa 
hawezi kuwa mpenzi wangu kwa sababu ni ndugu yangu ni binamu 
yangu,’’alisema Nay.
Shamsa naye alipoulizwa kuhusiano na picha hizo alisema ni filamu yao mpya wanafanya.             
 
 
 
 
          
      
 
  
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
No comments:
Post a Comment