DIAMOND, AUNT WAONGOZA SHANGWE ‘BIRTHDAY’ YA MOSE IYOBO

Mose Iyobo (kulia) akimlisha keki Diamond, usiku wa kuamkia leo ndani ya ukumbi wa Regence Hotel, Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Mose Iyobo akimlisha keki msanii wa filamu, JB.
Mmoja wa madansa wa Diamond aitwaye Dumy, akilishwa keki na Mose Iyobo.
Shamsa Ford hakuwa nyuma kula keki hiyo.

Baadhi ya waalikwa waliyojitokeza kwenye hafla hiyo wakimmwagia maji Mose Iyobo muda mfupi baada ya kuingia ukumbini hapo.
Diamond akifungua moja ya shampeni zilizoandaliwa mahususi kwa ajili ya hafla hiyo.
Mmoja wa waalikwa akimiminiwa shampeni na Diamond baada ya kuifungua.
Diamond akiwa amebeba keki.
Aunt Ezekiel na mzazi mwenzake,  Mose Iyobo, wakinywa shampeni.
Diamond akiandaa mazingira ya keki kabla ya zoezi la kuikata kuanza.
Keki ya sherehe hiyo.
Diamond akiongea jambo huku Mose na Aunt wakionekana kufurahia.
USIKU wa kuamkia leo dansa wa Crow ya Wasafi Classic Baby, Mose Iyobo, alisherehekea siku ya kuzaliwa kwake iliyohudhuriwa na  baadhi ya mastaa akiwemo bosi wake, Nasibu Abdul ‘Diamond’, na mzazi mwenzake, Aunt Ezekiel, ambapo kwa pamoja waliongoza shangwe kwenye pati hiyo.
Hafla hiyo ilifanyika ndani ya ukumbi wa hoteli ya Regence iliyoko Mikocheni jijini Dar es Salaam, ambapo mastaa na watu kibao  walihudhuria wakanywa na kukata keki iliyokuwa imeandaliwa maalum kwa sherehe hizo.

No comments:

Post a Comment