Kamishna Jenerali wa Magereza
Nchini, John Casmir Minja(pichani) kesho tarehe 20 Machi, 2015 saa 8:00
mchana atawavisha vyeo Maafisa wa Jeshi la Magereza wa ngazi mbalimbali
wa Mkoa wa Dar es Salaam waliopandishwa vyeo kwa mujibu wa Sheria.
Kwa Mamlaka aliyopewa kisheria na
Tume ya Polisi na Magereza ya Mwaka 1990, Kamishna Jenerali wa Magereza
Nchini atawavisha vyeo hivyo katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa wa
Magereza Ukonga, Jijini Dar es Salaam.
Tume ya Polisi na Magereza katika
Kikao chake Namba 2/2014/2015 kilichofanyika tarehe 16 Machi, 2015
chini ya Mwenyekiti Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Pereira
Ame Silima(Mb) imewapandisha vyeo Maafisa 292 wa ngazi mbalimbali
kuanzia tarehe 16 Machi, 2015.
Maafisa hao waliopandishwa vyeo ni Mrakibu Mwandamizi wa
Magereza kuwa Kamishna Msaidizi wa Magereza 11, Mrakibu wa Magereza kuwa
Mrakibu Mwandamizi wa Magereza 41, Mrakibu Msaidizi wa Magereza kuwa
Mrakibu wa Magereza 83 na Mkaguzi Msaidizi wa Magereza kuwa Mkaguzi wa
Magereza 157.
Imetolewa na; Inspekta Lucas Mboje, Afisa Habari wa Jeshi la Magereza,
Makao Makuu ya Jeshi la Magereza,
DAR ES SALAAM
19 Machi, 2015.
Makao Makuu ya Jeshi la Magereza,
DAR ES SALAAM
19 Machi, 2015.
No comments:
Post a Comment