
Bunge la Tanzania linaanza vikao vyake 
wiki ijayo, moja ya ishu ambayo wanasiasa na wanaharakati mbalimbali 
wamekuwa wakishinikiza kufanyiwa maamuzi ni ishu ya Escrow, mwezi 
DECEMBER, 2014 Rais Kikwete alitangaza kumsimamisha kazi Waziri Anna Tibaijuka kutokana na ishu ya fedha za Escrow ambazo kulikuwa na utata kwamba ni za umma ama za IPTL.
Vuguvugu lililobaki likawa kuwawajibisha
 Prof. Muhongo pamoja na Wenyeviti watatu wa Kamati za Bunge ambao 
walitajwa pia kuingiziwa pesa hizo, leo Prof. Muhongo ameitisha kikao na
 waandishi wa Habari ofisini kwake na kutangaza kujiuzulu nafasi ya 
Uwaziri.
Anakuwa Waziri wa pili kujiuzulu huku 
kukiwa na taarifa Magazetini leo kwamba Wenyeviti wa Kamati za Bunge nao
 pia wameachia nafasi hizo ili wachaguliwe wengine kabla ya Bunge kuanza
 Jumanne wiki ijayo.
endelea kufuatilia sakata hili kupitia tonytz.blog utafaham zaidi.
No comments:
Post a Comment