Shuwari itaendelea zaidi Gaza?


Watoto wa Gaza
Afisa wa serikali amesema kuwa Israel iko tayari kuzidisha kipindi cha kusitisha mapigano Gaza kwa saa kadha.
Makubaliano ya kusitisha mapigano kwa saa 12 yanatarajiwa kumalizika baada ya saa 2 za usiku za Afrika Mashariki.

Afisa huyo alisema muda huo huenda ukazidishwa kwa saa nne hadi usiku saa sita za Mashariki ya Kati.
Baraza la usalama la Israel linatarajiwa kukutana usiku.
Wakuu wa afya wa Gaza wanasema raia zaidi ya 1,000 wa Palestina, wengi raia, wameuwawa tangu mapigano ya sasa baina ya Israel na Hamas kuanza.
Maiti zaidi ya 80 zimekutikana chini ya vifusi wakati mapigano yaliposita.
Wanajeshi 40 wa Israeli wamekufa, pamoja na raia wawili na mfanyakazi kutoka Thailand.
Wakaazi wa Gaza wameingia mabarabarani kuchukua nafasi ya hali ya shuwari iliyopatikana.

No comments:

Post a Comment