
Marekani imefunga ubalozi wake wa Libya kwa muda na wafanyakazi wake wote wamehamishiwa nchi jirani, Tunisia.
Walipelekwa huko kwa magari huku wakilindwa na ndege za Marekani.
Wizara ya mashauri ya nchi za nje ya Marekani piya imewasihi raia wote wa Marekani waondoke nchini humo.
Jengo la ubalozi wa Marekani mjini Tripoli liko 
katika eneo ambalo limeathirika na mapambano kati ya makundi ya 
wapiganaji yanayozozana, ambayo yamekuwa yakigombania kudhibiti uwanja 
wa ndege wa kimataifa wa Libya.
Waziri wa mashauri ya nchi za nje, John Kerry, 
alisema kulikuwa na hatari hasa ikiwakabili wafanyakazi wa ubalozi huo, 
lakini alisisitiza kuwa shughuli za ubalozi zinasimamishwa kwa muda tu.
Miaka miwili iliyopita balozi wa Marekani 
aliuwawa pale ofisi ndogo ya ubalozi wa Marekani katika mji wa Benghazi,
 mashariki mwa Libya, iliposhambuliwa na wapiganaji Waislamu.
No comments:
Post a Comment