news:Diamond amefika Nigeria, soma na sikiliza sauti yake kuhusu alichoenda kufanya kinachomhusisha Iyanya na Davido
Diamond
Platinumz tayari ameshafika nchini Nigeria kwa ajili ya kazi ya
kimuziki pamoja na wasanii nchini humo ambapo baada ya kufanya remix ya
My Number One na Davido, kazi inaendelea na sasa amewafata hukohuko kwao
Nigeria.
Kila kitu kuhusu kilichompeleka huko Nigeria
Diamond anaelezea kwamba baada ya kufanya ngoma na Davido, pia ngoma
nyingine amefanya na Iyanya japokuwa watu wengi hawafahamu kuhusu hiyo
collabo. Lengo lake kubwa lilikuwa si kufanya collabo tu bali anasema
alitaka kujenga ukaribu na wasanii wa Nigeria ndiyo maana ameamua kwenda
kufanya video hukohuko Nigeria.
Japokuwa hajasema ni production gani atatumia, hivi sasa Diamond
ameshafika nchini Nigeria na atarudi baada ya kufanya video mbili ambapo
moja akiwa na Davido na nyingine pamoja na Iyanya.
No comments:
Post a Comment