Michuano
ya UEFA Champions League iliendelea hapo jana ikiwa kwenye sehemu yake
ya pili ya mzunguko wa pili wa hatua ya makundi .
Mabingwa
watetezi wa michuano hiyo Bayern Munich wakiwa ugenini kwenye uwanja wa
Etihad hawakuwa na huruma na vijana wa Manuel Pelegrini Manchester City
baada ya kuwafunga 3-1 .
Bayern
wanaoongozwa na Pep Guardiola walifunga kupitia kwa Frank Ribery ,Arjen
Robben na Thomas Mueller huku Alvaro Negredo akifunga bao la City .
Timu nyingine toka England Manchester United ambayo ilikuwa ugenini huko Ukraine ilitoka sare na Shakhtar Donetsk ambapo
timu hizo zilifungana bao 1-1. United walianza kufunga kupitia kwa
Danny Welbeck kabla ya kiungo Mbrazil Taison hajaisawazishia Shakhtar.
Mabingwa wa Ufaransa Paris St Germain wakiwa nyumbani kwao kwenye uwanja wa Parc-De-Princess
waliwafunga Benfica 3-0 . Wafungaji wa PSG walikuwa Zlatan Ibrahimovic
ambaye alifunga mabao mawili na Marquinhos .
Nao
Real Madrid waliwafunga Fc Copenhagen 4-0 kwenye uwanja wao wa nyumbani
Santiago Bernabeu . Cristiano Ronaldo na Angel De Maria walifunga mabao
mawili kila mmoja kwenye mchezo huo.
Katika
michezo mingine Juventus na Galatsasaray walitoka sare ya 2-2 katika
mchezo wa kwanza kwa Galatasaray tangu walipomuajiri kocha mpya Roberto
Mancini , CSKA Moscow nao walishinda mchezo wao dhidi ya Viktoria Plzen
kwa matokeo ya 3-2 , Bayer Leverkusen wakawafunga Real Sociedad 2-1 na Olympiakos wakaifunga Anderletch 3-0.
Story Za Michezo Kwa Hisani Ya Benki Ya NMB.
No comments:
Post a Comment