HATIMAYE MAN UNITED YANASA JEMBE LA KAZI FELLAINI KWA DAU LA PAUNI MILIONI 27.5!!


DAKIKA za lala salama za usajili wa majira ya kiangazi, hatimaye Manchester United imemnasa Marouane Fellaini  kutoka  Everton  kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni27.5.
Jaribio la United kutaka kumsajili nyota wa  Athletic Bilbao, kiungo  Ander Herrera liligonga mwamba baada ya timu hizo kushindwa kukubaliana dau la pauni milioni 30.5 kama ada ya kumnunua.
Sasa kocha wa Man United, David Moyes amekutana na kijana wake waliyekuwa wote Everton na kiukweli amemfukuzia kwa muda mrefu mpaka dakika za lala kwa buriani za usajili wa kiangazi barani Ulaya.
Reunited: Fellaini with manager Moyes after signing for Manchester UnitedWamekutana: Fellaini akiwa na bosi wake Moyes baada ya kusaini  Manchester United
Kiungo huyo wa Ubelgiji, Fellaini amekuwa akitakiwa kuungana na kocha wake wa zamani, Moyes na hakuwa na chaguo zaidi, isipokuwa kutua United.
Fellaini amepewa ruhusa ya kuchelewa kujiunga na kikosi chake cha timu yake ya taifa, ili kukamilisha uhamisho wake mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 kutua United, ambao ulikuwa unashughulikiwa na baba yake, Abdellatif.
United ilituma ofa tofauti kwa wote Fellaini na Leighton Baines mapema majira haya ya joto, ikianza na Pauni Milioni 28 jumla kwa wote na baadaye Milioni 36, ambazo zote zilipigwa chini na Everton.
Na inafahamika kwamba United ilijaribu kumsajili Mesut Ozil aliyetua Arsenal kwa Pauni Milioni 42 kutoka Real Madrid na ilitoa ofa iliyodunda na Pauni Milioni 34 kwa mchezaji mwingine wa Real, Sami Khedira kabla ya kujaribu kwa nyota wengine wa klabu hiyo Luka Modric bila mafanikio.
New man in town: Fellaini poses in a Manchester United shirtJembe jipya mjini: Fellaini akiwa amepozi na uzi wa  Manchester United 
Here he is: Fellaini arrives with Moyes at CarringtonLimewasili: Fellaini akiwasili na kocha wake  Moyes  maeneo ya Carrington

No comments:

Post a Comment