Unyanyasaji wa kinyumbani waharamishwa


Mfanyakazi wa nyumbani nchini Saudi Arabia
Serikali ya Saudi Arabia kwa mara ya kwanza imeanzisha sheria itakayoharamisha unyanyazaji na ukatili wa wafanyakazi wa nyumbani.

Lakini wanaharakati wa kutetea haki za kibinadam wana wasi wasi kuwa huenda sheria hiyo isitekelezwe kikamilifu.
Sheria hiyo ambayo vyombo vya habari nchini Saudi Arabia vinasema imeidhinishwa na baraza la mawaziri, itatoa hukumu ya kifungo cha mwaka mmoja gerezani na faini ya dola elfu kumi na tatu.
Hadi wakati huu, katika masuala ya sheria, dhuluma dhidi ya kina mama na watoto nyumbani imekuwa jambo la kibinafsi nchini Saudi Arabia
Wanaharakati wa kutetea haki za kibinadam wanasema hatua hiyo ni nzuri katika juhudi za kuhakikisha udumishwaji wa haki za kibinadam, lakini wanasema majaji na maafisa wa polisi wanahitaji mafunzo ili kuelewa masuala hayo.
Katika miaka ya hivi karibuni, idadi ya wafanyakazi wa nyumbani wanaodhulimiwa, nchini Saudi Arabia, wengi wao kutoka mataifa ya Kiafrika imekuwa ikiongezeka, hali iliyopelekea serikali za nchi kadhaa ikiwa ni pamoja na Kenya kupiga marufuku raia wake kwenda kufanya kazi za kinyumbani katika mataifa ya Kiarabu.

No comments:

Post a Comment