Jeshi la UN lafanya mashambulio Goma

Jeshi la Umoja wa Mataifa nchini Goma
Umoja wa Mataifa umesema ndege zake za kijeshi zilizoko Mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, zimefanya mashambulio dhidi ya waasi wa M-23 viungani mwa mji wa Goma.

Msemaji wa kijeshi wa Umoja wa Mataifa amewaambia waandishi wa habari kuwa ndege iliyofanya mashambulio, inamilikiwa na kitengo maalum kilichoundwa kukabiliana na waasi kwa ushirikiano na wanajeshi wa serikali ya Congo katika eneo hilo la Kaskazini mwa Goma.
Waasi wa M23 waliuteka na kuuthibiti mji huo wa Goma kwa muda mwaka uliopita na mapigano ya hivi karibuni yameongeza wasi wasi kuwa huenda waasi hao wakaishambulia tena mji huo.
Kikosi hicho maalum cha Umoja wa Mataifa kimepewa idhini ya kufanya mashambulio dhidi ya waasi ikiwa kutatokea haja ya kufanya hivyo.

No comments:

Post a Comment