Mwanajeshi wa Tanzania afariki dunia kwenye shambulio la bomu huko Congo


Home » Ent. » Mwanajeshi wa Tanzania afariki dunia kwenye shambulio la bomu huko Congo

3201Tanzania-flag

Wanajeshi wa Tanzania wanashiriki kwenye operesheni za Umoja wa Mataifa huko Goma DRC. Kikosi cha Tanzania kimeedelea na majukumu ya kulinda amani kama kinavyopangiwa na jeshi la pamoja la Umoja wa Mataifa huko Congo.

MONUSCO ndiyo jina la kikosi chenyewe na hivi karibuni kimepata shambulio la bomu wakati wanajeshi wapo kwenye eneo lao la ulinzi. Baada ya shambulio hilo wanajeshi waliojeruhiwa walikimbizwa hospitali kwa ajili ya matibabu na bahati mbaya mwanajeshi Major Khatibu Mshindo kutoka Tanzania alifariki njiani.Utaratibu  wa kuufikisha mwili wa marehemu nyumbani Tanzania, unafanywa na MONUSCO na utawasili hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment