Madame Rita na Ney wa mitego wakata maneno yawatu hadhalani,tazama picha zao zapamoja hapa chini.


vlcsnap-2013-08-29-14h05m34s162
Ni mengi umeyasikia wakati huu ikiwa ni siku kadhaa tu baada ya kutoa single ambayo amechana baadhi ya watu maarufu kwenye burudani na siasa Tanzania ambao Ney wa Mitego mwenyewe anasema lengo ni kufanya hivyo ili wajirekebishe.

Moja kati ya stori zilizotokea ni pale aliposema Madame Rita Paulsen amekwenda kumshitaki Mahakamani kisa katajwa kwenye wimbo ambao Ney aliuliza pesa za washindi wa BSS zinakwenda wapi, pia washindi hawafanikiwi kimaisha baada ya kutoka kwenye shindano hilo la kusaka vipaji vya uimbaji.
Sasa basi…… Ney wa Mitego na Madam Rita si wakakutana jana August 29 2013 kwenye uzinduzi wa video ya Diamond…………. unadhani walichuniana au kununiana? big Nooooo!!!!! walisimama, wakakumbatiana baada ya kuongea na hatimae kupiga picha ya pamoja wakiwa wanatabasamu…..
hii ilitokana na habari ambazo zilivyoandikwa ilionekana ni beef kati yao wawili manake Madame baadae alikanusha na kusema hakwenda kushtaki kokote na hawezi kufanya hivyo kwa sababu kwanza kilichosemwa na Ney sio kitu cha kupeleka na pia hajawahi kukutana na Ney na wala hamjui hata kwa sura.

vlcsnap-2013-08-30-00h19m14s136

vlcsnap-2013-08-30-00h19m17s193
vlcsnap-2013-08-30-00h19m27s28
vlcsnap-2013-08-30-00h19m46s225
vlcsnap-2013-08-30-00h19m50s19


No comments:

Post a Comment