MADEE ATEMBELEA KABURI LA NGWEA KIHONDA MKOANI MOROGORO

Mkali wa Bongo Fleva kutoka kundi la Tip Top Conection Madee ametembelea kaburi la mwanamuziki mwenzake Albert Mangwea aliyefariki dunia Mei mwaka huu Mjini Morogoro.
Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya mwanamuziki toka mkoani Morogoro Mwanaisha Nyange 'Dyna' kufanya hivyo siku chache zilizopita ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Madee alikuwa kwenye show mjini Morogoror katika ukumbi wa Nyumbani Park, ndipo baada ya kumaliza show yake, aliamua kutembelea na kufanya ibada katika kaburi la Mangwea.

No comments:

Post a Comment