Jezi namba 11 ya Bale Real Madrid yaingia sokoni.
Huku
wakiwa wanatajwa kuwa kwenye hatua za mwisho za kukamilisha usajili
wake toka klabu ya Tottenham Hotspurs klabu ya Real Madrid imeanza
kuziweka sokoni jezi zenye jina la mchezaji Gareth Bale .
Kwa
muda mrefu Real wamekuwa kwenye mazungumzo na Spurs kuhusu usajili wa
mchezaji huyu ambapo inaaminika kuwa Real wametenga dau ambalo
litamfanya mchezaji huyo kuwa mchezaji ghali kuliko wote duniani na
hakuna uficho kuwa rais wa Madrid Florentino Perez amekuwa akimsaka Bale
kwa udi na uvumba kwa muda mrefu.
Bale
amekuwa mkimya muda wote ambapo hajalizungumzia suala hili huku taarifa
za ndani zikisema kuwa ameshawaaga wachezaji wenzie wa Tottenham huku
pia akiwaambia wachezaji wenzie kwenye kambi ya timu ya taifa ya Wales
kuwa hatavaa jezi ya Spurs tena .
Jezi
za Gareth Bale zenye namba 11 mgongoni zimeingia rasmi sokoni wiki hii
nchini Hispania huku zikiwa tayari zimeshaanza kuuzwa mapema zaidi
kwenye kisiwa cha Gibraltar.
Mtandao
wa Real Madrid unaonyesha jina la Gareth Bale likiwa kwenye orodha ya
jezi ambazo mashabiki wa klabu hiyo wanaweza kuagiza.
Inaaminika
kuwa tayari makubaliano ya mauzo ya mchezaji huyo baina ya timu mbili
na mchezaji mwenyewe yamekwishamalizika na mchezaji huyo atathibitishwa
kuwa mchezaji wa Real siku si nyingi .
No comments:
Post a Comment