DILLISH WA NAMIBIA AIBUKA KIDEDEA BBA‘THE CHASE’2013


                         Dillish akiwa na mpenzi wake Steve
Fainali za Big Brother zimefikia tamati usiku wa jana Jumapili tarehe 25 August 2013 zikiwa na washiriki watano ambao ni Beverly wa Nigeri, Melvin wa Nigeria, Cleo wa Zambia, Elikem wa Ghana na Dillish wa Namibia.

Mshiriki kutoka nchini Namibia “Dillish” ndiye mshindi wa Big Brother Africa (the chase) alieondoka na dola 300,000 katika fainali zilizofanyika usiku wa jana Jumapili(August 25th).
Dillish mwenye miaka 24, hajawahi kuwa head of the house hata siku moja katika siku zote 91 alizokuwa ndani ya jumba, alishawahi kuwa nominated mara 5 na mara zote alibaki kwa kura za Africa, na hajawahi kuwa na mahusiano na mshiriki yoyote.
Dillish amekuwa ni mwanamke wa pili kushinda BBA tangu ilivyoanzishwa, baada ya Cherise kutoka Zambia kushinda kwenye BBA season 7 zilizopita
katka top 5 waliobaki, alianza kutoka Beverly (Nigeria), akafatia Melvin (Nigeria) na watatu kutoka ni Elikem (Ghana) wa nne ni Cleo (Zambia) na hatimae Dillish kuwa mshindi wa BBA The Chase 2013.
Mchujo huo uliwafanya Cleo na Dillish waingie katika masaa ya fainali za mwisho ambapo Cleo alielemewa na kutolewa huku akimwacha Dillish akichekelea $300,000 za ushindi wa shindano hilo....

Agalia jinsi kura zilivyopigwa:
Angola: Dillish
Botswana: Cleo
Ghana: Elikem
Kenya: Dillish
Ethiopia: Beverly
Malawi: Cleo
Namibia: Dillish
Nigeria: Melvin
South Africa: Cleo
Sierra Leone: Elikem
Tanzania: Dillish
Uganda: Dillish
Zambia: Cleo
Zimbabwe: Elikem
Rest of Africa: Melvin
Total:
Dillish = 5, Cleo = 4, Elikem = 3, Melvin = 2, Beverly = 1.

No comments:

Post a Comment