Kayumba wa B.S.S amkaanga Said Fela na zawadi yake ya milioni 50.

KUTANGAZA NASI, KUTUMA VIDEO NA AUDIO 


0684  524265


Kwenye mahojiano aliyofanya kwenye kipindi cha Planet Bongo EA Radio,mshindi huyo wa B.S.S ,2015-2016 amesema kisai cha fedha (milioni 50) alichozawadiwa bado kipo  ingawa kimepungua,tofauti na taarifa iliyotolewa Said Fela ambae ndie mlezi wa msanii huyo kupitia label yake ya ‘Mkubwa na wanae’,alienukuliwa na vyombo vya habari wiki chache zilizopita  kuwa fedha alizozawadiwa msanii huyo zimemalizika.

 
“Hela ipo, ingawa sio tena milioni 50,ntakua mwongo nikisema bado ipo milioni 50, lakini zipo siwezi kusema imebakia ngapi, si unaona napendeza nini, nyumba ipo kama nyumba zingine,siwezi kuzungumzia labda vyumba vingapi,ili mradi nitaweka ubavu wangu nitashukuru Mungu”.Alisema Kayumba.
kayumba na madam rita 00008
Kayumba (r)akiwa na Rita Paulsen,Mkurugenzi wa Benchmark Production,waandaji wa mashindano ya Bongo Star Search (BSS).
Taarifa imekuja zikiwa ni wiki chache tangu kusambaa kwa tetesi kwenye mitandao ya kijamii kuwa zawadi ya milioni 50 aliyopewa Kayumbaa baada ya kuibuka mshindi kwenye mashindanoi ya Bongo Star Search (B.S.S),kumalizika kuhu ujenzi wa nyumba ya msanii huyo ukiwa bado haujakamilika.

No comments:

Post a Comment