»Kalamu ya Nikki wa Pili: Hip Hop Inavyoikwamisha Hip hop Tanzania.

Image result for nikki wa pili 
Hip hop kwa upande wa kwanza ni CNN,BBC ama TBC(Sauti) ya mageto na mitaa mara nyingi ya watu wa chini. Na sehemu ya pili ni  fursa ya kuwatowa vijana magetoni na familia zao pia. Mfano kina jay z, luda, eminem, kanye, hawaishi tena kitaa ni matajiri wakubwa.

Hip hop Tanzania katika upande wa sauti ya mtaa imefanya kazi kubwa sana, toka nyimbo kama dei waka, mikononi mwa polisi, ndio mzee, chemsha bongo, good boy, show love, niaje ni vip, alikufa kwa ngoma nakadhalika. Kwakweli hamna jambo la kijamii ambalo hiphop haijaligusa, kuna maktaba ya kutosha itakayo somwa vizazi na vizazi kwa mana muziki  haufi.

Lakini katika upande wa kuwa fursa ya kuwatowa vijana bado haijafanya kazi kubwa kwa nini???
Haswa kipindi hichi ambacho biashara ya mziki inakuwa kubwa africa na bila shaka afro biti ndio mziki namba moja Africa.

Kuna mawazo miongoni mwa wana hiphop ambayo yana changanya na kupoteza mwelekeo wake, kwa ambao hawata  yatafakari.

kuwa hiphop ndio muziki wa kitaa lakini, ukiwa kitaani, bodaboda bajaji,saloon,clabu, masherehe kadhalika unaskia sana miziki ya kuimba moto, vanessa,barnaba, chache za rap. Sasa hicho kitaa tunachomanisha ni kipi??. Wakuimba wao hawaishi kwa imani wanapushi miziki yao kote kwenye harusi,mabaa,mageto, Magari, vipindi vya asubuhi mpaka usiku kote wamo.


Hip hop sio muziki wa media, lakini ndio wanaongoza kuwashambulia na kuwa lalamikia watu wa media na kuwatukana kwenye nyimbo? Ki vipi sasa na hiphop sio mziki wa media???.wakuimba wako bize kutafuta conection za media ndani na nje ya nchi.

Sisi ni hiphop wale sio, wale laini hawakazi, commercial lakinini!!!, hip hop si ni uhalisia wa mawazo ya mhusika, experience yake ya maisha aliyopitia, sasa unawezaje ku judge experience ya mtu na ukasema sio ya kweli(not real) wakati wewe hauja ipitia...ni upotezaji focus, lini umeskia  afro biti wanasema sisi ndio wale sio??

Ushindani wa kushambuliana utaskia, madogo wameteka gemu wakongwe wana hanya. Wakuimba wanashindana videos, colabo za kimataifa, mavazi nakadhalika vitu vinavyo ongeza thamani ya muziki.

Hip hop sio mziki wa biashara kweli?? 2pac kauza copi zaidi ya milioni 75, movies, mavazi kama rocawear, g unity, lable kubwa kama rock nation vyote hivyo vimefanyika kupitia hiphop jay z, ana zaidi ya doller milion mia 8, dre sasa ni bilionare. Waimbaji wanaongea biashara na kujaribu vitu vikubwa, hiphop inafursa kubwa lakini haya mawazo yatakwamisha wengi


Waimbaji wana, Bifu zisizo na madhara wanagombania mara wasichana ama mambo ya kiki na zinawapa media platform nakuwakuza, hiphop matusi tena mabaya, kutishiana mpaka kushambuliana na kuumizana, nakadhalika, ni kuiangusha

Anapotokea mwana hiphop anayetaka kujaribu mziki wake kufikia watu wengi na kuwa na matumizi mengi yani club, gheto, kwenye mabar, vipindi vyote, harusi. Watu wa kwanza kumvuta shati watakuwa wana hiphop, utaskia hakazi tena yule, ile laini, badala ya kumwona kama mtu anayetanuwa wigo,soko na kuongeza fan base na kufanya watu wengi kuwa karibu.na hip-hop

Kuzuia ubunifu wa ki style, biti, melodi, ushairi..katika hii dunia inayo kwenda kwa speed kali angalia matoleo ya simu yote ni kpata wateja wengi, kuboresha huduma na kufanya isichoshe watumiaji, angalia afro bit wanavyo.badili.kina wizkid, square, mondi, leo wamepiga densi hii kesho hii, mpaka wanaruka na para shoot kwa video...hiphop kivipi ibaki vile vile generation zinabadilika, dunia inabadilika jay cole hawezi kuwa Nas Wala 2Pac.

JE kusipokuwa na mifano ya wana HIP hop  waliofanikiwa? Mzazi gani ataruhusu mwanae afanye HIP hop na huo si ndio mwanzo wa kukosa vipaji vipya

Makala hii nimeandika kwa ajili ya wadogo zangu wenye kipaji huko form one. Msiwe kama sisi kuweni tofauti

Arakati ni pana staki kazi itakwambia ujiajiri, diamond, johmakini, vanesa watakuonesha kwa vitendo namna ya kujiajiri na wote hapo ni wana harakati kwa kuonesha jamii njia.

No comments:

Post a Comment