RAIS KIKWETE AWEKA JIWE LA MSINGI LA UJENZI WA DARAJA LA KILOMBERO
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akipungia wananchi kwa furaha wakati akielekea
ukingoni mwa Mto Kilombero kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa daraja la
kudumu juu ya mto Kilombero Agosti 20, 2014. Anaoongozana nao ni pamoja
na Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuri (kushoto kwa Rais), Waziri
wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Mbunge wa Ulanga
Mashariki Mhe. Celina Kombani (kulia), Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe.
Joel Bendera (kushoto) na Mama Salma Kikwete (nyuma ya Rais).
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akishangiliwa baada ya kuweka jiwe la msingi la
ujenzi wa daraja la kudumu juu ya mto Kilombero Agosti 20, 2014. Pamoja
naye ni Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuri (kushoto kwa Rais),
Waziri wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Mbunge wa
Ulanga Mashariki Mhe. Celina Kombani (kulia),Mbunge wa Ulanga Magharibi
Dkt Haji Ponda (kulia) na Mbunge wa Kilombero Mhe Abdul Mteketa (kulia
kwa Rais).
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo toka kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala
wa Barabara (TANROADS) Bw. Patrick Mfugale juu ya ujenzi wa daraja la
kudumu juu ya mto Kilombero Agosti 20, 2014. (kulia) ni Mama Salma Kikwete akifuatiwa na Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe, Magufuri
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe baada ya kuweka jiwe la msingi la
ujenzi wa daraja la kudumu juu ya mto Kilombero wilayani Kilombero mkoa
wa Morogoro Agosti 20, 2014. 
Magari
yakivuka juu ya daraja la muda la Mto Kilombero lililojengwa
kurahisisha kazi za ujenzi wa daraja la kudumu katika wilaya ya
Kilombero Mkoa wa Morogoro, wakati wa sherehe za uwekaji jiwe la msingi
wa ujenzi wa daraja hilo na Rais Jakaya Mrisho Kikwete Agosti 20, 2014.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wananchi baada ya kuweka jiwe la
msingi la ujenzi wa daraja la kudumu juu ya mto Kilombero wilayani
Kilombero mkoa wa Morogoro Agosti 20, 2014.
No comments:
Post a Comment