Hawa ndiyo waliopata tuzo majina na category zao yapo hapa #KTMA2014

                        Usiku wa Mei 3 ni usiku uliokuwa ukitolewa tuzo mbalimbali kwa wanamuziki waliofanya vizuri mwaka 2013/2014 huku usiku huu ukitawaliwa na burudani mbalimbali kutoka kwa wanamuziki wa Tanzania,hawa ni washindi waliofanikiwa kupata tuzo 2013/2014 kwenye category mbalimbali.

Katika Mtiririko huu wa Washindi Diamond Plutnumz ameweka historia nyingine mpya baada ya kuchukua jumla ya tuzo 7,cheki hapa chini.
1.Tuzo ya Wimbo bora wenye vionjo vya asili ya Tanzania ilichukuliwa na wimbo wa Bora Mchawi ya Dar Bongo Massive.
2.Tuzo ya msanii Bora chipukizi anayeibukia ilichukuliwa na Young Killer.
3.Tuzo ya wimbo bora wa Zouk imechukuliwa na wimbo wa Yahaya wa Lady Jay Dee.
4.Tuzo ya wimbo wa Afropop ni Number One ya Diamond Platnumz
5.Tuzo ya wimbo bora wa Ragga/Dancehall ni wimbo wa Nishai wa Juru ft. Tash.
6.Tuzo ya wimbo bora wa kiswahili ni Ushamba Mzigo ya Mashujaa Band.
7.Tuzo ya mwimbaji bora wa kiume taarab,mshindi ni Mzee Yusuph.
8.Tuzo ya mwimbaji bora wa kike Taarabu ni Isha Ramadhani.
9.Tuzo ya wimbo bora wa Taarab ni Wasi wasi wako wa Mzee Yusuph.
10.Tuzo ya wimbo bora wa Reggea imechukuliwa na wimbo wa Niwe na wewe ya Dabo.
11.Tuzo ya Mtunzi bora wa mwaka Hip hop imechukuliwa na Fid Q,
12.Tuzo ya wimbo bora wa kushirikisha/kushirikiana ni wimbo wa Muziki Gani ya Ney wa Mitego ft.Diamond.
13.Tuzo ya msanii bora wa Hip Hop imeenda kwa Fid Q.
14.Tuzo ya wimbo bora wa Hip Hop ni Nje ya Box ya Nikki wa Pili ft.Joh Makini na G nako.
15.Tuzo ya mwimbaji bora wa kiume kizazi kipya imeenda kwa Diamond Platnumz.
16.Tuzo ya mwimbaji bora wa kiume Bendi imeenda kwa Jose Mara.
17.Tuzo ya mwimbaji bora wa kike bendi ni Luiza Mbutu.
18.Tuzo ya wimbo bora wa R&B imechukuliwa na Closer ya Vanessa Mdee.
19.Tuzo ya kikundi cha mwaka imeenda kwa Weusi.
20.Tuzo ya mtunzi bora wa mwaka imeenda kwa Diamond Platnumz.
21.Tuzo ya mtunzi bora wa mwaka bendi ni Christian Bella.
22.Tuzo ya mtunzi bora wa mwaka taarab imeenda kwa Mzee Yusuph.
23.Tuzo ya wimbo bora wa Afrika Mashariki imechukuliwa na wimbo wa Tubonge wa Jose Chameleone.
24.Tuzo ya wimbo bora wa mwaka ni Number One ya Diamond Platnumz.
25.Tuzo ya heshima ya Hall of fame Institution imeenda kwa Masoud Masoud.
26.Tuzo ya heshima ya Hall of fame individual imeenda kwa Rehan Bitchuka.
27.Tuzo ya mtumbuizaji bora wa kike imeenda kwa Isha Ramadhani.
28.Tuzo ya wimbo bora wa mwaka ni Number One ya Diamond Platnumz.
29.Tuzo ya Mtayarishaji bora wa nyimbo za kizazi kipya ni Man Water.
30.Tuzo ya Mtayarishaji bora wa nyimbo wa bendi ni Amoroso.
31.Tuzo ya video bora ya Muziki ya Mwaka ni Number One ya Diamond Platnumz.
32.Tuzo ya kikundi bora cha mwaka Taarab ni Jahaz Modern Taarab.
33.Tuzo ya kikundi bora cha mwaka bendi ni Mashujaa.
34.Tuzo ya rapa bora wa bendi imeenda kwa Furgason
35.Tuzo ya Mtayarishaji bora wa mwaka taarabu imeenda kwa Enrico
36.Tuzo ya Mtumbuizaji bora wa kiume kizazi kipya ni Diamond Platnumz.
posted by  mussa fares monge  
  call +255 789346934 wats app +255 753967607
Instagram mussa faris msonge
tweeter mussa faris msonge 
facebook mussa faris.

No comments:

Post a Comment