Meno ya tembo 81 yakamatwa Tanzania

Watu wawili wanashikiliwa na polisi nchini Tanzania baada ya kukamatwa na shehena ya meno ya tembo katika bandari ya Dar es Salaam,
waliyokuwa wakisafirisha kiharamu maafisa wa nchi hiyo wamesema.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Wizara ya Maliasili na Utalii wa Tanzania, Chikambi Rumisha amesema meno hayo yapatayo 81 yana uzito wa kilo 303.
Kwa mujibu wa maafisa wa Wizara meno hayo ya tembo ni mapya ikiwa na maana yametokana na tembo 41 waliouawa ndani ya mwezi mmoja uliopita.
Naibu Waziri wa Maliasiali na Utalii wa Tanzania Lazaro Nyalandu amesema mauaji ya tembo yameongezeka nchini humo baada ya operesheni ya kupambana na majangili iliyopewa jina la "Operesheni Tokomeza" kusimamishwa kutokana na baadhi ya watendaji kukiuka haki za binadamu.
Mapema wiki hii Naibu Waziri huyo amesema tembo wapatao 60 wameuawa kati ya mwezi Novemba na Decemba ikilingalishwa na tembo wawili waliouawa mwezi Octoba.

No comments:

Post a Comment