KIFO CHA PAUL WALKER MAPYA YAIBUKA, MPENZI WAKE AJITOKEZA HADHARANI

 Jasmine Pilchard-Gosnell (23), alipowasili nyumbani kwa Paul Sant Barbara kwa ajili ya msiba.
Paul Walker enzi za uhai wake (kushoto) na Jasmine Pilchard-Gosnell.
Wakati watu wakiwa na huzuni bado kutokana na ajali iliyompata muigizaji mwenye mvuto wa Fast & Furious Paul Walker na kuchukua uhai wake, mapya mengine yameibuka kwa mujibu wa mtandao wa habari za mastaa huko majuu TMZ.
Paul mwenye miaka 40 imeelezwa amefariki kutokana na majeraha ya moto pamoja na ya ajali ya gari kujibamiza. Inasemekana wakati gari aina ya Porsche waliyopanda ilipopata ajali walikuwa hai bado lakini baada ya kuwaka moto ndipo walipopoteza uhai maana yake ni kwamba waliungua mpaka kufa.
Mpenzi wa siku nyingi wa Paul (40), Jasmine Pilchard-Gosnell (23) ameonekana hadharani kwa mara ya kwanza tangu ajali hiyo itokee alipowasili msibani Santa Barbara. Wapenzi hawa wamedumu kwa miaka 7 tangu walipoanza uhusino mwaka 2006 licha ya tofauti yao kiumri wakati huyo Jasmine ana miaka 16 na Paul 33 kwa hiyo utaona tofauti ya umri kati yao.

No comments:

Post a Comment