Vijana wadogo wanaovuta sigara.

Vijana wanaovuta sigara wako kati ya umri wa miaka 11-16
Michoro ya picha ya kwenye paketi za sigara ambayo inatoa onyo kali dhidi ya kuvuta sigara na kuonyesha madhara ya uvutaji sigara, hupuuzwa na vijana. Hii ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa nchini Uingereza.
Uingereza ilianza kutumia picha hizo ambazo zinaonyesha mapafu ambayo yemeathirika kutokana na moshi wa sigara pamoja na upasuaji wa moyo, mnamo mwaka 2008.

Lakini utafiti huo uliowahusisha watoto 2,800, uligundua kuwa picha hizo hazikuwazuia vijana wenye kati ya umri wa miaka 11 hadi 16 kununua na kuvuta sigara.
Hata hivyo, picha hizo ziligeuza maoni ya watu wasiovuta sigara na waraibu wa sigara.
Utafiti uliochapishwa katika jarida la kudhibiti matumizi ya Tumbaku ulidurusu data kutoka kwa utafiti uliofanyiwa vijana kuhusu utumizi wa sigara kabla na baada ya picha hizo kuanza kutumika kwenye paketi za sigara.
Kati ya watoto 2,800 waliohojiwa, mmoja kati ya watoto kumi alikuwa mvutaji wa sigara, wakati wengine walikuwa hawavuti sigara na wengine wakiwa wale waliowahi kujaribu kuvuta sigara.
Wakati idadi ya vijana waliofikiria kuwa onyo hizo zinaweza kuwazuia kuvuta sigara baada ya kuanza kutumiwa , miongoni mwao wale wanaovuta na wale wasio vuta, idadi ya wale waliojizuia kuvuta sigara kutokana na onyo za picha hizo ilipanda kwa asilimia moja kutoka kwa asilimia 13 hadi 14.
Mtafiti mkuu Daktari Crawford Moodie, alisema kuwa wakati jambo hili linaudhi kwamba picha zilizo kwenye paketi za sigara haziwezi kuwazuia vijana kuvuta sigara, idadi ndogo ya wale wanaotii onyo hizi sio mbaya sana.
Lakini pia alisema kulikuwa na tisho la watu kupuuza kabisa picha hizo na matamshi yanayoonya vikali dhidi ya uvutaji sigara, kwani picha hizo hazijabadilishwa tangu mwaka 2003 na 2008 mtawalia..
"nchi zengine hubadilisha picha na onyo dhidi ya uvutaji sigara mara kwa mara na baadhi wanahisi kuwa Uingereza inapaswa kuzibadilisha.

No comments:

Post a Comment