Obama aomba bunge kuidhinisha vita


Obama aomba idhini ya baraza la Congress kuhusu Syria
Haikuelekea kuwa Marekani itachukua hatua haraka ya kijeshi dhidi ya Syria, baada ya Rais Obama kuliomba bunge kuidhinisha shambulio.
Bunge halitaanza tena vikao hadi tarehe 9 September.
Mswada unaomba idhini ya bunge kutumia nguvu kuizuwia serikali ya Syria kutumia silaha za kemikali kwenye mashambulio.
Kuchelewa kwa ratiba ya Marekani piya kunawapa muda wakaguzi wa silaha wa Umoja wa Mataifa kumaliza uchunguzi ndani ya maabara.
Wakaguzi hao wamerudi na sampuli walizopata kwenye eneo linalodaiwa kuwa lilishambuliwa kwa silaha za kemikali, karibu na Damascus.

No comments:

Post a Comment