Hii ndio meli ya Tanzania iliyokamatwa nchini Italy ikiwa na shehena ya dawa za kulevya


Home » Ent. » Hii ndio meli ya Tanzania iliyokamatwa nchini Italy ikiwa na shehena ya dawa za kulevya


249316_577338042330194_1034080237_n
cegrab-20130907-235714-313-1-522x293Meli iitwayo Gold Star imekamatwa karibu na pwani ya Italy ikiwa na zaidi ya tani 30 za dawa za kulevya ambapo Polisi wa Italy wamesema documents zinaonyesha ilisajiliwa Tanzania.
Taarifa nyingine ya polisi imesema mzigo huo una thamani ya pound millioni 50 ambayo kwa pesa za kitanzania ni kama 126,582,278,481 na meli yenyewe ilikua na timu ya watu tisa ambao wanatoka Egypt na Syria na mzigo wote wameupakia kutoka Uturuki.
Unaambiwa baada ya kuona mchezo wao umefahamika, watu waliokuwemo kwenye meli waliamua kuanza kuichoma moto meli hiyo na wote tisa walijirusha baharini kwa nia ya kutaka kukimbia lakini wakakamatwa mapema tu na kukutwa na hizo dawa za kulevya aina ya hashish ambazo thamani yake inagonga kwenye £50m.
Bandari husika ya Italia walipewa taarifa kwa siri mapema siku kadhaa kwamba meli hii ilikua imebeba tani nyingi za dawa za kulevya hivyo wakawa wanaifatilia kwa siku kadhaa kabla ya kuikamata.
Msemaji wa bandari amesema hawakutegemea kama meli hiyo ingekua imebeba kiasi hicho cha dawa za kulevya na pia hawakutegemea kama watu waliokuwemo ndani yake wangeichoma moto ili kupoteza ushahidi japo zoezi hilo halikufanikiwa na dawa zikaonekana.
Meli hiyo imesogezwa kabisa mpaka kwenye bandari na moto umezimwa huku msako zaidi ukiendelea kwenye sehemu nyingine za meli hiyo ili kuona kama kuna dawa nyingine za kulevya huku watu wote tisa wakiwa wanaendelea kuhojiwa.

No comments:

Post a Comment