Interview ya Vanessa Mdee nyumbani kwake, amealikwa wapi? ‘closer’ inachezwa na station gani za nje?Vanessa Mdee TZANafahamu single ya ‘me and you’ aliyoshirikishwa na Ommy Dimpoz ndio ilifanya Tanzania ifahamu kwamba kuna nafasi mpya inamilikiwa rasmi kwenye bongofleva na mrembo anaitwa Vanessa Mdee.
Baada ya hapo alitoa single yake mwenyewe inaitwa ‘Closer’ ambayo kwa kipindi flani ilimfanya Vanessa Mdee kuwa mrembo pekee mwenye single on Clouds FM Top 20.

V Money anakwambia mbali na ‘Me and You’ kushinda kwenye KTMA 2013 ‘Closer’ pia imempa mafanikio zaidi kwenye kumtangaza, imemiliki chati za muziki na kumkutanisha na wasanii wengine ambao pia wametaka kolabo.
Kingine kikubwa kwa Vanessa Mdee ni kwamba anatarajia kuvuka mpaka na kwenda Congo DRC kuperfom kwenye harusi ya mtoto wa Rais, yani mke mtarajiwa single anayoipenda sana ni ‘Me and You’ ambapo hii itakua ni show yake kama ya tano kuifanya toka aanze kujulikana Tanzania.
Philadelphia
Philadelphia.
V ambae pia ni mtangazaji wa MTV Base na 102.5 Choice FM Dar es salaam kwenye interview na AyoTV alisema single yake mpya atakayoitoa soon itakua ikichezeka na video yake itafanywa Tanzania kwa sababu anaamini hapa kuna maeneo mengi mazuri sana ya kufanyia video japo watengenezaji wa video watatoka nje ya nchi.
Kwenye line nyingine, V amethibitisha kwamba single yake ya ‘Closer’ inachezwa kwenye radio za Kenya, Rwanda, Uganda, Burundi, South Africa kwenye online Radio, Philadephia Marekani kuna radio ambako V alionganishiwa na washkaji zake lakini pia TV maarufu ya SoundCity Nigeria na MTV Base video ya ‘Closer’ itaanza kuonekana.
Unaweza kumtazama V akiongea yote kwenye hii video ya AyoTV hapa chini.

No comments:

Post a Comment