Tazama maajabu haya Watu 3200 wakusanyika na kupigwa picha za utupu!

People take part in an installation titled Sea of Hull by artist Spencer Tunick 



Hull uingereza (1)     Hull uingereza (6)     Hull uingereza (11) 
Sehemu ya umati wa watu 3,200 waliohudhuria tukio hilo.
Hull, Uingereza
WATU zaidi ya 3200 wamekusanyika na kusherehekea utamaduni wao wakiwa kwenye huku wakiwa wamevua nguo zao zote (utupu) katika Mji wa Hull, Uingereza ikiwa ni tukio la kusherehekea mji huo kama Mji wa Utamaduni.
Hull uingereza (4)
Katika tukio hilo lilitokea Jumamosi ambapo washiriki walijipaka miili yao rangi ya bluu-baharina kisha kupigwa picha wakiwa katika maeneo mashuhuri jijini humo kama sehemu ya mradi uliopewa jina Sea of Hull.
Mradi huo unatekelezwa na mpiga picha Spencer Tunick na unadhaminiwa na taasisi ya Sanaa ya Ferens Art Gallery.
Hull uingereza (12)

Picha zilizopigwa siku ya tukio hilo, zitawekwa na kuoneshwa kwa umma wakati wa tamasha ya sanaa ya 2017 itakayoendelea kwa mwaka mmoja.
Hull uingereza (13)

Hull uingereza (7)
Tunick, anayetoka New York, amewahi kupiga picha za watu wengi wakiwa uchi Sydney Opera House, Place des Arts mjini Montreal, Mexico City na mjini Munich nchini Ujerumani Germany.
Hull uingereza (14)

Bw Tunick amesema kazi zake “hugusia historia ndefu ya Sanaa ya utupu”.
“Mavazi ni Sanaa ya mtu mwingine,” anasema.
Hull uingereza (15)
“Fashoni ni Sanaa. Kwa kuondoa hilo (mavazi), nitakuwa nafanya kazi na usawa na maumbile katika umaridadi wake.”
Hull uingereza (3) 
Bwana Tunick, kushoto, akisalimiana na mshiriki Stephane Janssen mwenye umri wa miaka 80.
Hull uingereza (8)Hull uingereza (5)
Watu karibu 3200 walijiandikisha kupigwa picha tangu wazo hilo litangazwe mwezi Machi mwaka huu huku Baraza la Mji wa Hull likifunga baadhi ya barabara wakati wa shughuli hiyo Jumamosi asubuhi.



No comments:

Post a Comment